Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitazama baadhi ya vifaa tiba vilivyopatikana kutokana na juhudi za
mbunge wa Geita vijijini, Joseph Msukuma (kulia) kwa ajili ya hospitali
ya wilaya ya Geita iliyopo katika kijiji cha Nzela, wakati alipokagua
ujenzi wa hospitali hiyo na kuzungumza na wananchi Septemba 21, 2019. Wa
pili kulia ni Mganga Mkuu wa wilya ya Geita, Deo Kisaka.(Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Vijana wa kijiji cha Nzela katika
jimbo la Geita Vijijini wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
wakati alipozungumza na wananchi baada ya kuakagua ujenzi wa hospitali
ya wilaya ya Geita, Septemba 21, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na wananchi baada ya kukagua ujenzi wa hospitali ya wilaya
ya Geita katika kijiji cha Nzela, Septemba 21, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
…………………………………………………
*Yaonesha kutoridhika na kasi, Waziri Mkuu atoa maagizo kwa NIDA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ameitaka Mamlaka ya Usajili wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ihakikishe
wananchi hasa walioko vijijini wanapata angalau namba za utambulisho wa
usajili wao kabla ya muda wa usajili wa laini za simu haujamalizika.
Ametoa agizo hilo jana (Jumamosi,
Septemba 21, 2019) wakati alizungumza na wananchi kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika uwanja wa hospitali ya wilaya ya Geita
iliyopo kwenye Kijiji cha Nzela.
Alisema kitendo cha kuwapatia
namba za utambulisho wa usajili wananchi ambao hawajapata vitambulisho
vya uraia kitawezesha kuingia kwenye orodha ya wale wanosubiri
kusajiliwa hata kama muda wa usajili utakuwa umeisha. Mwisho wa muda wa
usajili ni Desemba mwaka huu.
Waziri Mkuu alisema Serikali
imewapatia NIDA vifaa vya kisasa vya kielektroniki ili wafanye kazi zao
kwa haraka na ufanisi, lakini hali hairidhishi kwa sababu wananchi wengo
bado hawajapata vitambulisho na kasi ya usajili wa laini za simu
inalalamikiwa katika meneo mengi.
“NIDA mnalalamikiwa, nimeenda
Morogoro Vijijini NIDA mnalalamikiwa hivi utendaji wenu uko je? Kwanini
mnachelewa ?” Waziri Mkuu alimuuliza Afisa Msajili wa NIDA wa wilaya ya
Geita, Paschal Saro ambaye alijitetea kwamba wamesajili laini za simu
340 na tayari namba za usajili 330 zimeshatolewa.
Saro alimwambia Waziri Mkuu kuwa
suala la utata wa uraia kwa baadhi ya wananachi wanaoomba vitambulisho
vya NIDA ni moja ya sababu zinazochelewesha usajili wa vitambulisho vya
uraia.
Waziri Mkuu aliwasihi wananchi
wote kuwa walinzi wa nchi yao kwa kutoa taarifa za watu ambao wanaomba
viutambulisho vya uraia wa Tanzania wakati si raia na aliwataka watoe
taarifa mara moja kwenye vyombo vya dola pale wanapogundua kuwa kuna
raia wa nje anafanya mchakato wa kuapata vitambulisho hivyo.
Alisema katika baadhi ya mikoa ya
mipakani ambayo ina wakimbizi Serikali imekamata silaha ambazo raia
hawasurusiwi kuzimiliki na zinasadikiwa kuwa zimepenyezwa nchini na raia
wa nje wasiowaaminifu.
Awali,Waziri Mkuu, alikagua
ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Geita iliyopo katika kijiji cha Nzera
mkoani Geita na kufurahishwa na hatua ya Mbunge wa jimbo wa Geita
Vijijini, Joseph Musukuma ambaye amewezesha upatikanaji wa vifaa tiba
vya kisasa kwa ajili ya hospitali hiyo.
Waziri Mkuu alimpongeza Musukuma
kwa moyo wa upendo alionao kwa wapiga kura wake. Vifaa hivyo ni vya
kisasa na vinastahili kuwa katika hospitali za rufaa za mikoa lakini
mbunge huyo ameamua kuwapelekea wapiga kura wake kwenye hospitali ya
wilaya lengo likiwa ni kuboresha huduma.
0 comments:
Post a Comment