Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt.
Ashatu Kijaji akizungumza na wananchi wa wa Kijiji cha Mwongolo wilayani
Kondoa, ambapo wananchi hao walimuomba awatatulie kero ya maji ambayo
imekua changamoto kubwa kijijini hapo.
Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kondoa, Dodoma Alhaji Othman
Gora(kushoto) akiteta jambo na Katibu wa CCM Wilaya hiyo Bw. Nicholaus
Kasendamila wakati wa mkutano wa hadhara kati ya Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu
Kijaji na Wananchi wa Kijiji cha Mwolongo alipotembea Kijiji hicho.
Baadhi ya
Wananchi wa Kijiji cha Mwolongo wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt.
Ashatu Kijaji (hayupo pichani), alipokuwa anatolea majibu ya baadhi ya
changamoto zilizotolewa na wanakijiji hao.
Bi. Khadija
Irorya akimuelezea Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni
Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani),
changamoto ya ukosefu wa maji katika Kijiji hicho na kumuomba awasaidie
kuitatua kero hiyo iliyodumu kwa muda mrefu.
Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt.
Ashatu Kijaji akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Ilolo Bw. Ramadhani
Bakari alipotembea Kijiji hicho.
……………………
Na Mwandishi wetu, Kondoa
Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini
mkoani Dodoma Dkt. Ashatu Kijaji ameahidi kumaliza kero ya maji inayo
wakabili wakazi wa Kijiji cha Mwongolo mkoani humo.
Ametoa ahadi
hiyo alipokutana na wananchi wa kijiji hicho ambao walimweleza kuhusu
changamoto yao ya muda mrefu ya kukosa huduma ya maji safi na salama
pamoja na changamoto nyingine za ukosefu wa miundombinu mingine
inayoweza kuchochea kasi yao ya maendeleo.
Wananchi hao
walisema kero kubwa inayo waumiza ni upatikanaji wa maji katika kijiji
hicho ambapo wanawake wamekuwa wakilazimika kwenda umbali mrefu kuchota
maji jambo ambalo limewafanya kuchoka na kuhatarisha usalama wa maisha
yao.
Dkt. Kijaji
alisema kuwa amekuwa akichimba visima katika vijiji mbalimbali wilayani
humo ambapo hadi sasa jumla ya visima 65 vimeshakamilika na kutoa huduma
ya maji kwa wananchi.
“Leo
nimekamilisha kisima cha 65 Shule ya Msingi Kalamba niliposoma ndani ya
miaka minne ya uongozi wangu, hapa Mwongolo ni nyumbani na kwa mapenzi
niliyonayo kwa ndugu zangu wa Mwongolo, mhandisi akimaliza kuchimba
kisima cha kijiji cha Mwaisanga atakuja Mwolongo katika kipindi cha
mwezi huu au wa kumi kisima kitakuwa kimechimbwa” alisisitiza Dkt.
Kijaji.”
Aidha ameahidi
kufuatilia visima 14 vilichoahidiwa kuchimbwa kwenye sehemu ya machinjio
ya kijiji hicho na Wizara ya Maji kupitia Wakala wa Uchimbaji Visima na
Mabwawa, (DDCA), ili nao waweze kupata maji kwa ajili ya shughuli zao
za kila siku.
Aliongeza kuwa
Serikali ya Awamu ya Tano ni sikivu hivyo itaendelea kuboresha huduma
mbalimbali za jamii kama vile Sekta ya elimu, huduma za afya, nishati,
maji, miundombinu ili ziweze kuwafikia wananchi wote nchini kwa urahisi
zaidi.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwolongo Bw. Miraji Ramadhani, amemshukuru
Dkt. Ashatu Kijaji kwa kutenga muda wa kwenda kutembelea kijiji hicho na
kutatua baadhi ya kero zilizokuwa vinawasumbua muda mrefu.
Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ameahidi hadi kufikia 2020 vijiji
vyote 84 vya Jimbo lake la Kondoa Vijijini vitakua vimepata huduma ya
maji kwa njia ya visima vya maji ili kumaliza kabisa kero ya maji
Jimboni humo.
0 comments:
Post a Comment