Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Edward Mpogolo amewataka wahandisi wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanatoa
ushauri katika kila mradi unaojengwa kwa nguvu za wananchi.
DC Mpogolo amesema ni jambo la
kushangaza kuona wananchi wanamuunga mkono Rais Dk John Magufuli kwa
kushirikiana na Serikali kujenga miradi mbalimbali halafu hawapati
ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wahandisi.
Hayo ameyasema wakati wa ziara
yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi
anayoifanya kwenye Wilaya hiyo.
DC Mpogolo amesema toka ameanza
ziara hiyo na kukagua baadhi ya miradi inayojengwa kwa nguvu za wananchi
vikiwemo vyumba vya madarasa hakuna sehemu yeyote ambayo wahandisi
wamefika na kutoa ushauri wao.
” Hakuna mradi wenye nguvu za
wananchi ambao watalaamu letu wamefika na kutoa ushauri. Hivyo nawaagiza
kutoka ofisini na kuja huku kushauri kuliko Wananchi wanatumia nguvu na
kidato chao halafu watumishi wanaopaswa kuwahudumia wao wamekaa tu
ofisini.
” Nimepita kwenye mashule,
zahanati kote huko watalaamu hawajafika, wanasubiri fedha zinazotoka juu
kwa kuwa zina posho hii wanaiacha kwa kuwa haina posho, sasa natoa
agizo na litekelezwe,” Amesema DC Mpogolo.
Aidha amewataka wataalamu hao
kupita kwenye miradi yote iliyopo kwenye Kata za Wilaya hiyo na kumletea
ripoti inayoonesha miradi waliyoitolea ushauri.
0 comments:
Post a Comment