Wakazi wa
Jiji la Mwanza wakiwemo waumini wa dini mbalimbali wameendelea kujitokeza kwa
wingi kwenye mkutano mkubwa wa injili ulioandaliwa na kanisa la kanisa EAGT
Lumala Mpya chini ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kukola.
Jana mamia
ya wananchi walijitokeza kwenye mkutano huo unaofanyika kwenye uwanja wa
Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza na kukutana na mlipuko mkubwa wa injili kutoka
kwa watumishi wa Mungu akiwemo mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani chini
ya huduma ya MORE International Ministry.
Aidha waimbaji
Ambwene Mwasongwe, Mbilikimo Watatu, Samwel Lusekelo, Joseph Rwiza, Sam D,
Havillah Gospel Singers na wengine wengi wameendelea kukonga nyoyo za
wahudhuriaji kwenye mkutano huo.
“Maandalizi
ya mkutano huu ni ya kuvutia, tuna majukwaa matatu makubwa, vyombo vya muziki wa
injili vizuri na pia tunatoa zawadi mbalimbali ikiwemo vyakula na nguo kwa
wanaohudhuria mkutano huu”. Alisema Mchungaji Dkt.Kulola na kuwahimiza watu
wote kufika kwenye mkutano huo ili wakutane na nguvu ya Mungu na kufunguliwa.
Mkutano huo
ulianza juzi jumatano Septemba 27 na utafikia tamati jumapili Oktoba Mosi, 2017
katika Uwanja wa Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza ambapo mamia ya wananchi
waliokuwa wakiteswa na majini pamoja na magonjwa mbalimbali wanazidi kufunguliwa,
na leo huduma ya maombezi inaanza mapema majira ya saa nne asubuhi na mkutano
utaanza saa tisa alasiri hadi saa 12 jioni.
Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani akihubiri kwenye mkutano huo
Watumishi mbalimbali wakiendelea kutoa huduma ya maombezi jana ambapo zaidi ya 20 walifunguliwa mapepo huku wengine wengi wakiponywa magonjwa mbalimbali
Mwimbaji wa muziki wa injili Ambwene Mwasongwe kutoka Dar es salaam akihudumu kwenye mkutano ho
Baada ya ibada, kanisa la EAGT Lumala Mpya kwa kushirikiana na wachungaji kutoka Marekani lilitoa zawadi kwa wananchi
0 comments:
Post a Comment