Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Bodi na
Menejimenti ya NBC na Mabenki mengine kuwa kuanzia sasa Taasisi zote za
fedha ziweke kipaumbele cha kwanza katika kuwezesha kuendeleza viwanda
nchini hasa viwanda vidogo vidogo na vya kati vya kuongeza thamani ya
mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, misitu na madini ambayo yanapatikana kwa
wingi hapa nchini.Pia viwanda ambavyo vinatumia teknolojia ya kati na
nguvu kazi zaidi ( labour intensive technology).
Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akihutubua kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya NBC.
Mhe. Samia alisema mabenki mengi yameendelea kutoza riba
ubwa hivyo kupelekea wananchi wa kipato cha chini hivyo aliwataka
Wataalamu wa NBC na Sekta za Fedha kwa ujumla kutafuta suluhisho la riba
zisizo rafiki kwa walio wengi ili amana pamoja na mikopo iweze
kuongezeka.
Makamu wa Rais aliziagiza Bodi na Menejimeni ya NBC na
Mabenki yote nchini kuzingatia Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha,
alisema ” Serikali ya Tanzania haitomuonea mtu haya na itachukua hatua
kali dhidi ya benki au Taasisi yeyote itakayobainika kukiuka matakwa ya
sheria hiyo.”
Mwisho Makamu wa Rais aliipongeza benki ya NBC kwa kuweza
kutoa gawio la Shilingi Bikioni 1.2 mwaka huu 2017 kwa mara ya kwanza
tangu kuanzishwa kwake.
0 comments:
Post a Comment