METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, July 31, 2019

CCM YAPIGA MARUFUKU UJAZAJI WA RUMBESA NA VIPIMO VYA UJAZO WA MAZAO USIOZINGATIA HAKI KWA WAKULIMA NCHINI


Dkt Bashiru Ally akizungumza wana CCM katika mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilemela tarehe 30 Julai 2019 kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama  cha Mapinduzi kama ilivyoahidiwa na Mbunge wa Jimbo hilo wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilemela tarehe 30 Julai 2019 kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015.
Sehemu ya wana CCM wakifuatilia mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilemela tarehe 30 Julai 2019 kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt Bashiru Ally (wa sita kushoto), Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa Kheri James (wan ne kushoto), Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Anthony Dialo ( wa nne kulia) wakipiga makofi wakati wa mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilemela tarehe 30 Julai 2019 kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa Kheri James wakicheza na mmoja wa wana kikundi cha ngoma wakati wa mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilemela tarehe 30 Julai 2019 kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilemela tarehe 30 Julai 2019 kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015.

 ...........................

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally amehudhuria Mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilemela  wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya CCM Jimbo la Ilemela-uwanja wa CCM Kirumba.

Mkutano huo maalum wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani, uliofanywa na Mbunge wa Ilemela Mama Angelina Mabula umehudhuriwa viongozi mbalimbali wa chama na serikali wakiongozwa Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Ndg. Kheri James Mwenyekiti wa Vijana wa CCM taifa na Mama Munde Tambwe, mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ndg. Jamal Babu, viongozi wa Mkoa, Wilaya, Kata, Matawi na wajumbe wote wa mashina  Wilaya ya Ilemela.

Katibu Mkuu akizungumza katika mkutano huo, ametoa maelekezo kwa viongozi wa serikali hasa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kusimamia vipimo vya ujazo wa mazao ikiwemo kupiga marufuku ujazaji wa rumbesa na mizani isiyotenda haki kwa wakulima.

"Natoa maelekezo nchi nzima kwa wakuu wa mikoa na wilaya kwa niaba ya CCM, kama mnataka kazi ndani ya serikali hii ya CCM nisisikie malalamiko kuhusu ujazaji wa rumbesa kama ambavyo baadhi ya wafanyabiashara wanawafanyia wakulima wetu hivi sasa.  Rumbesa, na mizani isiyokuwa ya haki kwa wakulima wetu ni kosa kisheria, na kamati za siasa za mikoa, wilaya, kata na matawi simamieni hili na mtoe taarifa ili wananchi wanyonge wasiendelee kunyanyaswa." Dk. Bashiru ameelekeza.

Wakati huo huo, Ndg. Kheri James akimkaribisha Katibu Mkuu, amewataka vijana wote nchini kuendelea kuwatetea viongozi kwa nguvu zote dhidi ya baadhi ya watu wasio itakia mema nchi yetu kwa kutoa kejeli na kuwakatisha tamaa viongozi wetu, licha ya kazi kubwa wanayoifanya kwa nchi yetu.

"Ninawaomba vijana nchi nzima, tuendelee kuwalinda viongozi wa chama na serikali dhidi ya yeyote anayetoa kejeli kwa kazi kubwa wanazofanya viongozi wetu usiku na mchana, hatutaruhusu mwenyekiti na Rais wetu, Katibu Mkuu wetu na viongozi wote wakatishwe tamaa na watu wachache wasioitakia mema nchi yetu."  Ndg. Kheri amesisitiza.

Ziara hii ya siku tano, imeanza leo Mkoani Mwanza ikiwa ni muendelezo wa kutekeleza jukumu la viongozi wa CCM kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com