METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, July 31, 2017

WADAU WA MAENDELEO KUTOKA KOREA KUSINI WAITHIBITISHIA ILEMELA USHIRIKIANO ZAIDI KATIKA MAENDELEO

Wadau wa maendeleo kutoka nchini Korea ya Kusini wameithibitishia Ilemela ushirikiano zaidi katika kuhakikisha inapata maendeleo ya haraka kwa wananchi wake kupitia Imani ya Kijiji cha Mfano (Semaul Spirit)

Hayo yamebainishwa leo na kiongozi wa Ugeni huo Profesa Lee, Kyeong-Soo wakati akizungumza na timu ya maendeleo kutoka wilayani Ilemela mapema mara baada ya kuwasili wilayani hapo kwaajili ya kutembelea maeneo mbalimbali yanayotarajiwa kutekelezwa miradi ya maendeleo

‘…Tunashukuru sana kwa ukarimu na mapokezi yenu, tunapenda kuwathibitishia kuwa tutaendelea kushirikiana na Ilemela kuhakikisha  tunatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni ukamilishaji wa imani yetu kwa vitendo ya uwajibikaji, ushirikishaji na kujitoa (Semaul Community) …’ Alisema

Ugeni huo mapema leo umefanikiwa kufanya mazungumzo na Mhe John Mongela Mkuu wa mkoa wa Mwanza kabla ya kutembelea Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela  na baadae kituo cha afya cha Sangabuye na kuhitimisha katika Mradi wa Vijana wa Kilimo unaotekelezwa chini ya The Angeline Foundation kwa kushirikiana na Manispaa ya Ilemela 

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mhe Renatus Mulunga sambamba na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Wanga mbali na kushukuru kwa Ugeni huo kwa kuja Ilemela wamewahakikishia kuwa Ilemela itaendelea kuwa sehemu salama na rafiki kwa Uwekezaji na Utekelezaji wa shughuliza maendeleo sambamba na kufikisha salamu za Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula ambaye ndio muasisi wa mashirikiano kati ya Jimbo la Ilemela na Wadau hao wa Maendeleo
Hapo kesho Ugeni huu unataraji kuelekea Kata ya Sangabuye Kijiji cha Ihalalo unapotekelezwa mradi wa Kijiji  

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
31.07.2017
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com