Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine
Mndeme akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama waliokuwa wakichota maji.
1Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine
Mndeme akifurahi jambo na wafadhili wa mradi wa maji wa Mhande kutoka Canada.
1Wananchi wa Mhande wakimsikiliza Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma Chritine Mndeme katika uzinduzi wa mradi wa maji wa kijiji
hicho.
1Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine
Mndeme pamoja na Father Fransis wakifungua bomba la maji kama ishara ya
uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mhande.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine
Mndeme akisalimiana na father Fransis
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine
Mndeme akiteta jambo na Brother Anthony ambaye ni muasisi wa mradi wa CPPS.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme
akikagua eneo la pampu ya maji ya mradi
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme
akicheza ngoma baada ya kuzindua mradi wa maji.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme
akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mhande
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme
akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mhande
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine
Mndeme akifurahi jambo na akina mama wa kijiji cha Mhande
1 Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine
Mndeme akiwa ameketi katika mmoja ya kaya za wakazi wa Mhande akipata chakula
baada ya kuzindua mradi wa maji.
................................................................................
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Christine Mndeme leo amezindua
mradi wa Maji katika kijiji cha Mhande,Kata ya Ngh'ong'hona ambao umefadhiliwa
na Shirika shirika la wamishionari wa damu takatifu ya Yesu(CPPS) uliogharimu kiasi cha Sh.Milioni 35.
Mradi huu umetokana na maombi ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini
Anthony Mavunde kwa Shirika la hilo kusaidia kutatua changamoto ya Maji katika
kata hii ya Ngh'ongh'ona ambayo wananchi wake wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo
kubwa la upatikanaji maji safi na salama.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mndeme amelishukuru shirika
hilo la CPPS kwa ufadhili wa mradi huo na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma
Mjini Anthony Mavunde kwa kuwa mstari wa mbele kutatua kero za wanachi wake
hususani kero kubwa ya Maji katika kata ya Ngh'ongh'ona.
Amesema kutatuliwa kwa kero hiyo kumewatua kina mama ndoo
kichwani kwa kuwa walikuwa wakienda kuchota maji umbali mrefu.
“Mwili unahitaji maji unapotafuta maji mbali roho inasononeka
hata muda wa kusali unaukosa, tunashukuru sana shirika hili lakini wananchi
tuna wajibu wa kuutunza mradi huu ambao ni wa thamani kubwa sana,”amesema
Hata hivyo amesema hatasita kuwachukulia hatua watu
watakaoharibu miundombinu ya mradi huo wa maji huku akiwataka kuunda kamati ya
maji ili kuendesha mradi huo.
Aidha amesema kwa kushirikiana na Mavunde watashughulikia
upatikanaji wa umeme katika mradi huo wa maji ili uweze kutoa huduma ipasavyo
kwa wananchi.
Naye, Diwani wa Kata hiyo Philipo Edward amesema wananchi hao
wamekuwa wakipata adha kubwa ya maji na kulazimika kutembea umbali wa zaidi ya
kilomita 10 kufuata huduma hiyo vijiji jirani jambo lilosababisha kushindwa
kufanya shughuli za kimaendeleo.
0 comments:
Post a Comment