Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (wa
kwanza kushoto) akimkabidhi Mbunge wa Kyela ambaye pia ni Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe injini ya boti iliyotolewa
na Serikali kwa ajili ya kikundi cha wavuvi cha Kyela mkoani Mbeya wakati wa
hafla ya makabidhiano ya injini hiyo leo jijini Dodoma.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (wa pili
kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kaliua Abel Yeji Busalama injini ya boti
iliyotolewa na Serikali kwa ajili ya kikundi cha wavuvi wilayani humo wakati wa
hafla ya makabidhiano ya injini hiyo leo jijini Dodoma.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (wa pili
kushoto) akimkabidhi Mbunge wa Mtwara Vijinini Hawa Ghasia (wa kwanza kulia)
moja ya injini ya boti kati ya mbili zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya
kikundi cha Vita Fishing group cha Msanga Mkuu na Kikundi cha Jiwezeshe cha
Nanyumbu vya mkoni Mtwara wakati wa hafla ya makabidhiano ya injini hizo leo
jijini Dodoma.
Serikali
kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekabidhi injini nane za boti awamu ya pili
kwa wabunge wa majimbo mbalimbali kwa lengo la kuvipatia vikundi vya ushirika
vya uvuvi vilivyopo katika majimbo yao ili kusawaidia kuboresha utendaji kazi
wao na kufanya shughuli za uvuvi wenye tija.
Awali
wizara hiyo ilitoa injini za boti tano na kufanya jumla ya injini zilizotolewa
na wizara hiyo kufikia 13 ambazo jumla zimegharimu kiasi cha Sh. milioni 60.
Akikabidhi
injini hizo za boti leo jijini Dodoma, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina
amesema kuwa Wizara yake inahimiza vyama vingine vya ushirika viboreshe
utendaji wao wa kazi ili navyo viweze kupata ruzuku ya Serikali.
“Mtakubaliana
na mimi kwamba wavuvi wetu wengi wanatumia zana duni sana na wanashindwa
kufanya kazi zao za uvuvi kutokana na zana duni wanazotumia katika uvuvi na
kutokana na zana zao hizo kuwa duni wanafanya kazi miaka nenda rudi lakini
maisha yao hayabadiliki kutokana wanachopata ni kwa ajili ya chakula tu”
alisema Waziri Mpina.
Ili kujua
changamoto za wavuvi nchini, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanya tahmini kwa
kuzunguka nchi nzima kujionea wananchi wanavyoendesha shughulizao za uvuvi
ikiwemo changamoto wanazokutana nazo ambapo wamefanikiwa kuwaunganisha wavuvi
katika vyama na vikundi mbalimbali ambavyo vinasaidia kurahisisha utendaji kazi
ikiwemo kupata ruzuku kutoka Serikalini hatua inayowasaidia kufanya shughuli za
uvuvi wenye tija kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Akitolea
mfano wa vikundi vilivyonufaika na mikopo, Waziri Mpina alisema kuwa Wilaya ya
Ukerewe imefanikiwa kuwa na vikundi vya wavuvi ambao wamenufaika na mikopo ya
zaidi ya Sh. milioni 500 na kufanya vyama vya ushirika nchini kufanikiwa
kukopeshwa na taasisi za fedha zaidi ya sh. milioni 800.
Kwa upande
wake Mbunge wa Kyela na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.
Harrison Mwakyembe amesema kuwa wavuvi nchini wameanza kuchangamkia fursa
zinazotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano hatua ambayo itawafanya wawe na mafanikio
makubwa kiuchumi.
Dkt.
Mwakyembe alifafanua kuwa wilaya ya Kyelea ina mito mikubwa ya kudumu mine
ikiwemo Kiwira, Songwe, Lufilio na Mbaka pamoja na ziwa Nyasa, lakini mazao ya
samaki wilayani humo ni duni kutokana na mifaa duni vya uvuvi, hivyo injini ya
boti aliyokabidhiwa itawasaidia wavuvi kuwa na uvuvi ambao utawasaidia kupata
samaki wengi ambao watakidhi mahitaji ya soko.
Amesema
injini hiyo itawasaidia wavuvi kuvua kiutaalamu zaidi na kwa usalama
ikizingatiwa ziwa Nyasa kuna samaki wakubwa aina ya Mbasa ambao ni wakubwa
kupita mitumbwi ya kawaida ambayo inatumiwa na wavuvi hao.
“Nina
uhakika Wanakyela watahamasika kujiunga kwenye vikundi vya ushirika, wakulima
hao hao wa Kyela ni sehemu ya wavuvi, wataunda vikundi imara, tutoke kwenye umasikini,
tuongeze zaidi tija na mbinu za kisasa” alisema Dkt. Mwakyembe.
Aidha, Dkt.
Mwakyembe amemthibitihia Waziri Mpina kuwa injini hiyo itawafikia wananchi na
itatunzwa ili iweze kuwa na manufaa zaidi kwa wananchi wa Kyela.
Naye Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatama amesema
kuwa wavuvi wadogo wadogo wanachukua asilimia 85 ya wavuvi wote nchini ambapo
samaki wote wanovuliwa ni karibu asilimia 90 wanavuliwa na wavuvi wadogo.
Katika
mwaka 2019/2020, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetambua vyama vya ushirika vya
wavuvi vipatavyo 102 katika mikoa yote nchini hatua ambyo imesaidia pia
kuhamasisha kuanzishwa vyama vipya 14 na kufanya jumla ya vyama vya ushirika
vinavyotambuliwa na wizara hiyo kufuikia 116.
Lengo la
kuanzishwa vyama hivyo ni kuwawezesha wavuvi na wakuzaji viumbe maji kuwa na
sauti ya pamoja ili waweze kupata mikopo na masoko ya bidhaa zao.
Vyama vya ushirika vilivyopata injini hizo za
boti ni Magawa, Kisiju, Shungubweni vya mkoa wa Pwani, Mwamapuri wilaya ya Igunga
mkoani Tabora, Mbamba Bay wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, kikundi cha wavuvi
Kyela mkoani Mbeya, kikundi cha Vita Fishing group Msanga Mkuu na Kikundi cha
Jiwezeshe cha Nanyumbu mkoni Mtwara, Wakulima wa mwani Kwaigoma wilaya ya
Handeni mkoani Tanga, Bukasige Finshing Cooperative society cha Ukerewe mkoani
Mwanza, kikundi cha wavuvi cha Nyamikoma cha Busega na kikundi cha wavuvi cha
Kasanga Kalambo wanaofanya shaghuli zao eneo la ziwa Tanganyika.
0 comments:
Post a Comment