Baraza kuu
la waislamu Tanzania (BAKWATA) wilaya ya Ilemela limempongeza mbunge wa jimbo
hilo Mhe Dkt Angeline Mabula kwa kujali na kuthamini, wajane, yatima, wazee,
walimu wa dini ya kiislamu, mashekh, masikini na watu wasiojiweza katika
kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Kauli hiyo imetolewa na shekh wa wilaya ya Ilemela Husein Mwamba katika viwanja vya shule ya msingi Kitangiri
wakati wa zoezi la ugawaji sadaka ya futari kwa wagane, wajane, yatima, wazee,
walemavu na watu wasiokuwa na uwezo kutoka kata 19 za wilaya ya Ilemela ambapo
shekh huyo amempongeza mbunge Dkt Mabula kwa kujitoa kusaidia watu wasiokuwa na
uwezo huku akiwataka viongozi wengine na wadau kuona haja ya kusaidia makundi
maalum katika jamii yenye uhitaji.
‘.. Waislamu wapo katika ibada ya kutekeleza amri ya mola wao, Kwa mapenzi
makubwa akaona walau apate wazee, mayatima, wajane na wale wasiojiweza ili atoe
sadaka kuwawezesha watekeleza ibada yao kwa salama na amani, Mbunge hakuangalia
kabila, dini wala rangi wapo wenye uwezo
wa kupata futari na wapo wasioweza, Tuna wajibu wa kumuombea dua na kumpongeza
..’ Alisema
Aidha shekh huyo akawataka waislamu hao kushukuru kwa futari iliyotolewa na
kuendelea kumuombea dua mbunge huyo kwa moyo wake wa kujali na kushirikiana na
jamii katika mambo mbalimbali huku akikiri kupokea barakoa na ndoo 42
zitakazogawanywa katika misikiti yote iliyopo ndani ya wilaya hiyo kama sehemu
ya kujikinga na ugonjwa wa virusi vya Corona zilizotolewa na mbunge huyo.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amewashukuru
wadau alioshirikiana nao katika kufanikisha utoaji wa sadaka hiyo akiwemo
mkurugenzi wa GBP Ndugu Rashid Seif Sudi, Mr Brown Mteta Peter wa Nakiete
Pharmacy ya Dar es Salaam, Olympic Petroleum, Charles Mlowa wa Tropical
Company, Samuel Melishek Mollel wa Nakoroi Ltd Dar es Salaam, KCB Bank Tanzania
Ltd, Princes Pharmaceutical Ltd na Tarmal Industries Ltd huku akitoa fursa kwa
wadau wengine watakaohitaji kushirikiana nae katika kusaidia utatuzi wa kero na
changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.
Akihitimisha katibu wa BAKWATA wilaya ya
Ilemela Shekh Sadick Mchora mbali na kumpongeza mbunge huyo akaongeza
kuwa ipo haja kwa waislamu na viongozi wa dini kuendelea kukumbushana juu ya
kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Covid-19 ili kuzuia maambukizi mapya ya
ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment