Na; Ramadhani Shabani, Dodoma
Ndugu Mtanzania Ni Tumaini Langu Wewe Ni Buheri Wa Afya Na Unaendelea Vyema Na Utekelezaji Wa Majukumu Yako Ya Utekelezaji Wa Kauli Mbiu Ya Hapa Kazi Tu!Ikiwa Ina Hamasisha Utendaji Wa Kazi Kwa Bidii Kwa Maendeleo Ya Taifa Letu.
Ndugu Mtanzania Kama Ilivyokuwa Hada Yetu Kukuletea Habari Ya Mambo Mbalimbali Ambayo Yamekuwa Yakijiri, Na Sasa Leo Tumekuletea Hii Ya Vijana Wa CCM Ambao Ni Wanadhuoni Wa Vyuo Na Vyuo Vikuu Ikiwa Ni Moja Ya Idara Iliyochini Ya (UVCCM) Ambao Wamekuwa Wakijifunza Na Kupata Darasa La Itikadi Ya Chama Chao Ambalo Linaendelea Ktk Chuo Cha Serikali Za Mitaa (Hombolo) Wilayani Dodoma Mjini Mkoani Dodoma.
Ndugu Mtanzania Kambi Hilo Liloanza Mapema Siku Ya Ijumaa 23/06/2017 Na Kufunguliwa Na Mhe Katibu Wa Nec Siasa Na Uenezi Ndugu *Humphrey Polepole*Ambaye Alizungumzia Maswala Mbalimbali Huku Akisisitiza Na Kuwasihi Vijana Wa Idara Ya Vyuo Na Vyuo Vikuu(UVCCM) Ambayo Inasimamiwa Na Ndugu *Daniel Zenda*Kuakikisha Kwamba Wanasema Na Kujitokeza Wazi Kabisa Kuunga Mkono Juhudi Ambazo Amekuwa Akifanya *Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli*Kwa Uzalendo Wake Wa Kuzipigania Na Kuzirinda Rasilimali Za Taifa Letu.Mhe Polepole Alikwenda Mbali Zaidi Kwa Kuwasihi Vijana Hao Kwamba Vita Anayopambana Sio Ya Kwake Pekee Bali Ni Ya Wana CCM Sambamba Na Watanzania Wote Kwa Maslahi Mapana Ya Taifa Letu.*Mhe Polepole Ambaye Hapo Siku Ya Ijumaa 23/06/2017 Baada Ya Kufungua Kambi Hilo Alielekea Mkoani Mwanza Kwaajili Ya Kushiriki Shughuli Maalum Iliyokuwa Imeandaliwa Na Wananchi Wa Mkoa Huo Wa Mwanza Na Kulenga Kuunga Mkono Juhudi Za Mhe Rais Magufuli Katika Kupigania Na Kutetea Rasilimali Za Taifa Letu.
Ndugu Mtanzania Kama Hii Haitoshi Kambi Hilo Liliendelea Hapo Siku Ya Jana Kwa Watoa Mada Mbalimbali Wakiongozwa Na Mhe Katibu Wa Nec Siasa Na Uhusiano Wa Kimataifa Ndugu *Kanali Mstaafu Kapteni Ngemela Lubinga*Ambaye Alitoa Mada Ya Uzalendo Na Uongozi.Ukiachana Na Kapteni Lubiga Watoaji Mada Wengine Leo Walikuwa Ni Makomrade Vijana Wakiongozwa Na Katibu Wa Idara Ya Vyuo Na Vyuo Vikuu Ndugu *Daniel Zenda*
Ndugu Mtanzania Kambi Hilo Limepambwa Sana Na Burudani Ya Nyimbo Maalum Za Kizalendo Za Chama Chetu (CCM) Ambapo Nyimbo Hizo Za Kizalendo Na Hamasa Zimekuwa Zikiimbishwa Na Muhamasishaji Na Mwimbaji Maarufu Sana Na Mtaalam Wa Uimbishaji Na Utungaji Wa Nyimbo Hizo Ndugu *Hassan Nyange*Aka Mwl Nyange.
Ndugu Mtanzania Kauli Mbiu Ya CCM Mpya Na Tanzania Mpya Ina Maana Kubwa Sana Na Malengo Yake Makubwa Yamekuwa Yakilenga Ktk Kukirejesha Chama Chetu Hiki Ktk Misingi Ambayo Inakifanya Chama Kuwa Cha Wanachama Na Ambacho Misingi Yake Inasimamia Haki Kwa Wanachama Wote Kwa Usawa Bila Ubaguzi.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Kidumuuu chama Cha Mapinduzi
ReplyDeleteKidumuuu chama Cha Mapinduzi
ReplyDelete