METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, June 24, 2017

NDG DEBORA CHARLES ACHANGIA LAKI MOJA NA ELFU AROBAINI MAHAFALI YA TATU USCF TAWI LA CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO

Na; Mwandishi wetu, Dar es Salaam.

Katibu Msaidizi Mkuu Sera, Utafiti, Itikadi na Uenezi UVCCM Taifa Ndg. Debora Charles leo Jumamosi 24/05/2017 amehudhuria Mahafali ya tatu ya Tawi la University Students' Christian Fellowship (USCF) Chuo Kikuu cha Bagamoyo na kuchangia kiasi cha shillingi laki moja na elfu arobaini (140,000) kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za Tawi hilo.

Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wahitimu wa chuo hicho sambamba na wageni waalikwa ilifanyika katika ukumbi wa Kanisa la Kiinjili na Kirutheri  Tanzania (KKKT) Kinondoni.

Katika hafla hiyo ambapo Ndg. Debora alikuwa ndio mgeni rasmi kwa kigezo alichonacho kama mmoja wa waanzilishi wa Tawi hilo lililozinduliwa rasmi 24/05/2015 na Rais wa USCF Taifa wa wakati huo, matukio mbalimbali yalifanyika yakiwemo kugawa vyeti kwa wahitimu, kuimba pamoja na kumuabudu Mungu.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Ndg. Debora alisema vijana hawana budi kufanya kazi kwa bidii sambamba na kumuunga mkono Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake yote.

*_"Vijana hususani nyinyi wasomi ni hazina kubwa kwa Taifa , lazima mfanye kazi kwa bidii sambamba na kumuunga mkono Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa Juhudi kubwa anazozifanya katika kuuinua Uchumi wa nchi yetu "_* alisema Ndg. Debora na kuendelea;-

*_"Ukiiangalia Bajeti ya mwaka 2017/2018 kuna kodi nyingi zimeondolewa na nyingine kupunguzwa, hili lina maana kubwa katika kumpunguzia gharama za Uzalishaji Mtanzania wa kawaida hususani Mkulima",_*alisema Debora.

Pia wakati wa hafla hiyo ilifanyika harambee iliyoongozwa na Ndg. Debora Charles yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kuendeleza Tawi hilo ambapo kiasi cha shillingi laki tano na elfu mbili mia tano *(502500/=)* kilipatikana.

Akizungumza baada ya hafla hiyo mmoja wa wahitimu hao Mwinjilisti Christopher S. Kivuyo alimshukuru Ndg. Debora kwa moyo wake wa kuitikia wito bila kipingamizi sambamba na kuchangia kiasi cha pesa jambo ambalo wao  hawakulitarajia.Katibu Msaidizi Mkuu Sera, Utafiti, Itikadi na Uenezi UVCCM Taifa Ndg. Debora Charles akihutubia katika Mahafali ya tatu ya Tawi la University Students' Christian Fellowship (USCF) Chuo Kikuu cha Bagamoyo Katibu Msaidizi Mkuu Sera, Utafiti, Itikadi na Uenezi UVCCM Taifa Ndg. Debora Charles Akimtunuku cheti mwenyekiti mstaafu wa tawi la USCF Chuo kikuu cha Bagamoyo  katika Mahafali ya tatu ya Tawi la University Students' Christian Fellowship (USCF) Chuo Kikuu cha Bagamoyo Ndg Justin Barnabas MwakitajaKatibu Msaidizi Mkuu Sera, Utafiti, Itikadi na Uenezi UVCCM Taifa Ndg. Debora Charles Akicheza mziki wa injili wakati wa kusifu na kuabudu katika Mahafali ya tatu ya Tawi la University Students' Christian Fellowship (USCF) Chuo Kikuu cha Bagamoyo.Katibu Msaidizi Mkuu Sera, Utafiti, Itikadi na Uenezi UVCCM Taifa Ndg. Debora Charles akikabidhi keki kwa washiriki katika Mahafali ya tatu ya Tawi la University Students' Christian Fellowship (USCF) Chuo Kikuu cha BagamoyoKatibu Msaidizi Mkuu Sera, Utafiti, Itikadi na Uenezi UVCCM Taifa Ndg. Debora Charles (Wapili kulia), wengine ni Ebeneza Emmanuel na Nachzongo Jonathan na Mwenyekiti Mteule wa Tawi la University Students' Christian Fellowship (USCF) Chuo Kikuu cha Bagamoyo Ndg Laurence SafariKatibu Msaidizi Mkuu Sera, Utafiti, Itikadi na Uenezi UVCCM Taifa Ndg. Debora Charles akimkabidhi Cheti mwinjilisti wa  Tawi la University Students' Christian Fellowship (USCF) Chuo Kikuu cha Bagamoyo Ndg Christopher Kivuyo

Share:

1 comment:

  1. Hakika sherehe ilipendeza sana. Tunamshukuru Mungu kwa kuifanikisha. Wahitimu wote zingatieni "Kuongeza thamani katika utu wenu" kama ambavyo mafundisho yalivyoelekeza.

    ReplyDelete

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com