Yanga yajiweka pabaya Klabu Bingwa Afrika
Zanako FC wameilazimisha Yanga sare ya kufungana goli 1-1 kwenye uwanja wa taifa katika mchezo wa klabu bingwa Afrika.
Yanga wakiwa kwenye uwanja wa taifa wamelazimishwa sare ya pili kwenye michuano hiyo baada ya kutoka sare ya kufungana goli 1-1 na N’gaya Club ya Comoro.
Simon Msuva alianza kuifungia Yanga goli la kuongoza dakika 39 kipindi cha kwanza baada ya Ngoma kumpasia Justine Zulu ambaye aliuweka mpira kwenye njia Msuva akaukuta na kuunganisha kwa mguu wake wa kushoto kuiandika Yanga bao.
Zanaco walipata bao la kusawazisha mnamo dakika ya 77 lililofungwa na Attram Kwame akiwa pekeake kwenye nje kidogo ya sita baada ya kupigwa mipira miwili mirefu ambayo mabeki wa Yanga walishindwa kuidhibiti.
Matokeo hayo sio mazuri kwa upande wa Yanga kwa sababu watalazimika kupata ushindi wa magoli yoyote au sare ya kuanzia magoli mawili na kuendelea ili kufuzu hatua inayofata.
The post Yanga yajiweka pabaya Klabu Bingwa Afrika appeared first on Zanzibar24.
Zanzibar 24
0 comments:
Post a Comment