Majaji wa mahakama ya katiba nchini
Korea Kusini, wakati walipotoa hukumu kuhusu kumuondoa madarakani Park
Geun-hye. Machi 10, 2017.
Majaji wa mahakama ya katiba kwa kauli
moja wameidhinisha uamuzi wa bunge la nchi hiyo kumuondoa madarakani
rais Geun-hye, kutokana na ushiriki wake katika masuala ya rushwa
yakimuhusisha rafiki yake wa karibu Choi Soon-sil.
Kwa uamuzi huu sasa, inamaana kuwa anapoteza kinga zote za urais alizokuwa nazo na huenda akakabiliwa na mashtaka.
Wafuasi wa rais Park Geun-hye ambaye sasa amevuliwa madaraka yake rasmi kutokana na uamuzi wa mahakama ya katiba.
Kumeshuhudiwa makabiliano ya polisi na
wafuasi wa Park nje ya mahakama ya katiba, ambapo wafuasi wake wanapinga
kiongozi wao kuondolewa madarakani na wanapinga uamuzi huu wa mahakama.
Shirika la habari la Korea Kusini
Yonhap, limeripoti kuwa watu wawili wamekufa, akiwemo mzee mmoja ambaye
alianguka kutoka kwenye gari la polisi, hata hivyo taarifa zaidi bado
zinaendelea kuibuka.
Uamuzi huu wa mahakama ni hitimisha la miezi kadhaa ya maandamano yaliyoanza mwaka jana dhidi ya utawala wa rais Park Geun-hye
Park alisimamishwa kazi za urais toka
mwezi Desemba mwaka jana baada ya bunge kupiga kura kutaka aondoke
marakani, huku waziri mkuu akikaimu majukumu yake.
Kwa uamuzi huu wa mahakama una maanisha
kuwa nchik ya Korea Kusini itahitajika kuchagua rais mwingine mwanzoni
mwa mwezi Mei mwaka huu.
Kwa wakati huu rafiki wa Park, Choi
ameshashtakiwa kwa makosa ya kutoa hongo na kwamba alitoa shinikizo kwa
makampuni makubwa kutoa fedha ili yapate msamaha wa Serikali, rais Park
amekuwa akituhumiwa kujihusisha kwenye kashfa hii.RFI
0 comments:
Post a Comment