Juzi Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari
kupitia umbrela yao iitwayo "Jukwaa La Wahariri" walisafirishwa kwenda
kuonana na Eddo. Gharama za usafiri, chakula, malazi, communication
allowance etc, zililipwa na Eddo mwenyewe.
Jana wakafanya nae
Press Conference, lakini yaliyotokea huko ni aibu tupu. Nimeona baadhi
ya maswali waliyouliza wahariri hao kwa Eddo nikatokea kuwadharau sana.
Moja ya swali lililoulizwa na Hamis Dambaya ni hili, "Mheshimiwa Kuna
watu wanaandika juu ya afya yako kutetereka, lakini sisi tunakuona fit
ndio maana umetuita hapa.. je unalisemeaje hili?"
Hahahaa.!
Nimecheka sana.. Hivi ni swali gani hili? Hili ni swali la kuulizwa na
mwandishi wa habari? Tena Hamis Dambaya aliyebobea katika taaluma ya
Habari kwa kiwango cha Masters katika Mass Communication?
Mwingine akauliza eti "kuna watu wanakuita Eddo badala ya kukuita kwa
hadhi yako Mhe.Edward Lowassa. Na wewe umekua ukiitika hata unapoitwa
Eddo, Je huoni hii ni kupunguza heshima yako ktk jamii?"
Hivi
swali gani hili? Lowassa kuitwa Eddo au kuitwa Edward kunahusiana vp na
hatma ya nchi yetu ikiwa atakua Rais? Tulitegemea maswali "critical"
yenye kupima uwezo wa Lowassa kuongoza nchi hii sio kuhoji eti
anajisikiaje akiitwa "Eddo"..
Hii ni mifano tu lakini maswali yote yaliyoulizwa ni ya hovyo hovyo na yanayoonesha wazi kuwa it was just "agenda setting".
Ni ugoigoi wa kiwango cha PhD kudhani Lowassa anapoteza heshima yake
akiitwa "Eddo" au Kikwete atapoteza heshima yake kwa kuitwa "JK" au
kudhani Nyerere alipoteza heshima yake kwa kuitwa "Mwalimu". Ikiwa
mnaona hivyo, basi kamwambieni mimi naendelea kumuita "Eddo".
Nimekerwa sana na aina ya maswali waliyoiluliza wahariri.
Ieleweke sipingi nia ya Eddo kugombea urais wa nchi hii. Eddo kama
mtanzania yeyote yule ana haki ya kugombea na kama watanzania watampa
ridhaa ana haki ya kutuongoza.
Nachopinga ni "ugoigoi
uliotukuka" wa waandishi wenzangu waliokubali kugeuzwa misukule ya
wanasiasa na kufikia kugeuka mazuzu. Waandishi wa aina hii hawafai
kuendelea kuwepo kwenye "industry" ya habari.
Wazungu husema "the
one who decide what you eat can decide what to speak". Yani anayeamua
nini ule ndiye anayeamua nini uongee. Nimeona yametimia kwa Jukwaa la
wahariri.
Waswahili nao husema "anayemlipa mpiga zumari ndiye
anayechagua wimbo".. Eddo amewalipa wahariri na amewachagulia maswali ya
kumuuliza. This is shame.!
Najiuliza hivi kama Wahariri
wamekubali kugeuzwa "condom" na kutumika hovyo, vipi waandishi wa
kawaida ambao wengi wao ni maskini wa kutupwa?? Wale ambao ukiwaita
kwenye event yako wanachukua hotuba ya mgeni rasmi na kunyoosha mkono
uwape chochote kisha wanaondoka kwenda kuwahi event nyingine..
Yesu alipokua msalabani aliwauliza wale wayahudi "ikiwa mmeutenda hivi mti mbichi, itakuaje kwa mti mkavu?"
Na mimi najiuliza ikiwa wahariri wamekubali kununuliwa kama bidhaa,
itakuaje kwa waandishi wa kawaida? Wahariri wengi wana nyumba, mathalani
makazi ya kueleweka. Wana magari, na mishahara yao si haba.
Lakini Waandishi wengi ni "pangu pakavu". Waajiri wanawanyonya sana kwa
kuwalipa mishahara kiduchu. Hawana makazi ya kueleweka.. Leo utamkuta
Manzeshe kesho Yombo Buzza. Usafiri wao ni huu wa umma wa "mama Uledi
simama vizuri nipate pa kujishika". Sasa hawa kweli watashindwa
kununulika tena kwa bei chee?
Kuna wakati niliwahi kusema tasnia ya habari haiwezi kubadilika kamwe kwa sababu sisi tunaotakiwa kuleta Mabadiliko
hatujielewi. Leo waandishi wanapiga kelele sana mishahara midogo lakini
hawako tayari kuungana kutetea maslahi yso. Uoga umewazidi, wanaishia
kununuliwa.
Waandishi wengi wanaishi kwa kuunga unga kama treni
ya tazara. Mishahara yao ni aibu hata kutaja. Kuna baadhi yao hata
mishahara hawapewi. Wanaishi kwa "tip". Ukiandika story unasubiri story
yako itoke. Ikiwa Mhariri ataipitisha itoke utalipwa elfu 10 kwa story.
Hivi huyu mwandishi anaishije?
Halafu badala ya kuungana kupambania maslahi yao wanakubali kunuliwa kama nyanya na vitunguu vya Ruaha Mbuyuni. This is shame.!
Nimelidharau sn Jukwaa la Wahariri. Hiki ndicho chombo pekee
kilichopaswa kuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya waandishi lakini
wamewageuka, wamewasaliti, wamewasahau wenzao.
Nashauri Jukwaa
Hili livunjwe. Na ikiwa kweli Waandishi wako "serious" na wanaumizwa na
kukandamizwa na maslahi duni wanayopata, nashauri waungane na kulikataa
"Jukwaa feki, Jukwaa la Wachumia Tumbo, Jukwaa la wapenda fursa, jukwaa
la wahariri"
Malisa GJ || Your Partner In Critical Thinking.!
0 comments:
Post a Comment