Dk. Gudila Valentine akiwasilisha mada
kuhusu ugonjwa wa Figo katika kongamano la kitaaluma ikiwa ni
maadhimisho ya siku ya Figo Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka
Machi 9.
Baadhi ya Madaktari na wauguzi wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali
kuhusu magonjwa ya Figo zilizowasilishwa katika kongamano hilo leo .
Wauguzi wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili wakimuhudumia mgonjwa katika kitengo cha Figo, kushoto ni
kiongozi wa kitengo hicho Sister Judith Mwaipopo na kulia ni Sister
Lucy Kyombo.
Watanzania wametakiwa kuepuka utumiaji holela wa dawa za maumivu ili kuepuka uwezekano wa kupata magonjwa ya Figo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es
salaam na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Figo wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili Jakline Shoo alipokua akiwasilisha mada katika maadhimisha
siku ya figo Duniani, katika kongamano la kitaaluma lililofanyika leo
katika ukumbi wa CPL uliopo ndani ya Hospitali hiyo.
Akifafanua Dk. Shoo amesema ni vema
watu wakaepuka matumizi holela ya dawa za maumivu kwani ni chanzo cha
magonjwa ya figo lakini pia kuepuka unene uliokithiri kwa kula mlo
bora na kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa ya Kisukari na shinikizo la
damu ambayo yanachangia mtu kupata ugonjwa sugu wa figo.
Akielezea kuhusu wagonjwa wanaohudumiwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Shoo amesema katika Kiliniki
yao kwa kila mwezi huwaona wagonjwa watu wazima kati ya 120 hadi 150 .
Pia takwimu zinaonyesha kuwa asilimia
10 ya watu Duniani tayari wanaugua ugonjwa sugu wa figo na kwamba
inakadiriwa ifikapo mwaka 2025 asilimia 70 ya wagonjwa watakua wanatokea
katika nchi zilizopo Ukanda wa Jangwa la Sahara.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya
Figo Duniani mwaka huu ni ugonjwa wa figo na uzito uliozidi , mienendo
bora ya maisha kwa ajili ya afya bora ya Figo.
0 comments:
Post a Comment