Na Carlos Nichombe
BARAZA la Michezo la Taifa(BMT)
limewataka wadau wa michezo mbalimbali hapa nchini kuacha kasumba ya
kuwategemea wadau kutoka jiji la Dar es Salaam katika kuongoza shughuli
za vyama vyao.
Ofisa Habari wa Baraza hilo, Najaha
Bakari amesema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wadau kuhisi kwamba watu
wenye uwezo wa kushika nyadhifa za juu kwenye vyama vyao ni kutoka Dar
es Salaam jambo ambalo linazidi kushusha maendeleo ya mpira hapa nchini.
Amesema kiongozi bora hatokani na mkoa
anaotokea bali kinachotazamwa zaidi ni elimu pamoja na udhoefu ambao
umewekwa na chama cha mchezo husika na sio kwamba wanakuwa wanaangalia
eneo ambalo analotokea mdau anayetaka kugombea nafasi hizo.
Kauli hiyo ya Najaha imetolewa ikiwa ni
siku chache zimepita tangu zoezi la uchukuaji fomu wa chama cha mchezo
wa MASHUA ulipokamilika huku ikibainika idadi kubwa ya wagombea wa
nyadhifa za juu wakitokea katika mkoa wa Dar es Salaam.
Amedai kitendo cha wadau wa mchezo wa
mashua kutoka mikoa tofauti na Dar es Salaam kuogopa kugombea nyadhifa
za juu kinaendeleza dhana potofu iliyojengeka kwa miaka mingi iliyopita.
“Ifike mahali wadau wa michezo hapa
nchini tubadili mawazo yetu na tuone kwamba kila mtu mwenye sifa
zilizoorodheshwa na vyama wakati wa uchaguzi anahaki ya kugombea nafasi
yoyote ya uchaguzi pasipo kujali yeye ametokea mkoa gani na kama wadau
hao watafanya hivyo ni imani yangu michezo itazidi kukua zaidi tofauti
na sasa,” amesema Najaha.
Hata hivyo Najaha ameendelea
kusikitishwa na mwenendo wa zoezi la uchukuaji fomu za kuwania nafasi
mbalimbali za uongozi wa chama cha MASHUA ambalo limemalizika hivi
karibuni na kudai hali ya ushindani katika uchaguzi huo inatarajiwa kuwa
ni ndogo kuliko ilivyokuwa ikitarajiwa hapo awali
0 comments:
Post a Comment