Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Terminal 1 Jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Oktoba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera wakati nyimbo za Mataifa mawili ya Tanzania na Malawi zikipigwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Terminal 1 Jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Oktoba 2020.

Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus
McCarthy Chakwera akikagua Gwaride la Heshma lililoandaliwa na Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Terminal 1 Jijini Dar es Salaam leo tarehe
07 Oktoba 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia mgeni wake Rais wa Jamhuri ya
Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera zawadi ya picha ya Mlima
Kilimanjaro mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 07
Oktoba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Oktoba 2020. PICHA NA IKULU.
0 comments:
Post a Comment