Bruno Le Roux Desemba 22, 2016.
Ofisi ya mashitaka mjini Paris imetangaza kumchunguza Waziri wa Mambo
ya Ndani nchini Ufaransa Bruno Le Roux baada ya madai kuwa, aliwaajiri
mabinti wake wawili kama wasaidizi wake alipokuwa mbunge.
Bw Le Roux baada ya kupokelewa na rais
wa Ufaransa François Hollande ena Bernard Cazeneuve, alitangaza
kujiuzulu kwenye nafasi yake aliyokua akishikilia kwa kipindi
kisichozidi miezi minne. Katibu Dola Matthias Fekl ameteuliwa kuchukua
nafasi yake.
Le Roux mwenye umri wa miaka 51,
anakutana na Waziri Mkuu Bernard Cazeneuve baadaye sikuy ya Jumanne,
kujieleza kuhusu madai haya.
Kituo cha Habari cha TMC, kimeripoti
kuwa Le Roux wakati akiwa Mhunge aliwaajiri mabinti wake kati ya mwaka
2009 na 2016 na kuwalipa Dola za Marekani 59,000.
Madai haya yamewakumbusha raia wa
Ufaransa kuhusu Francois Fillon mgombea urais nchini humo kupitia chama
cha Republican ambaye pia amedaiwa.
Licha ya madai haya, sheria nchini
Ufaransa inawaruhusu wabunge kuwaajiri watu wa Familia zao ikiwa
watafanya kazi itakayotambuliwa.
Hata hivyo, Fillion na sasa Le Roux
kutoka chama cha Kisosholisti wanadaiwa kutoa ajira hizo lakini watu wao
wa Familia hawakufanya kazi kama ilivyodaiwa.RFI
0 comments:
Post a Comment