Ndugu zangu,
Inahusu
umuhimu wa kupanga mambo yetu. Inahusu muda na matumizi ya muda. Na
mwanadamu usipokuwa makini na muda, itakuwa sawa na kisa kile cha mzazi
aliyeulizwa na wanawe; " Mbona nguo za Krismasi hatujanunuliwa?"
Mzazi akawajibu wanawe; " Jamani, Krismasi ya mwaka huu imekuja ghafla sana!"
Kana kwamba hakujua, kuwa kwenye kalenda ya mwaka tarehe ya Krismasi imeshawekwa, Desemba 25!
Kana kwamba hakujua, kuwa kwenye kalenda ya mwaka tarehe ya Krismasi imeshawekwa, Desemba 25!
Ndio,
Afrika mvua hainyeshi ghafla, huwa kuna dalili zake. Na katika maisha,
mambo mengi hayaji ghafla, bali hutukuta tukiwa hatujajiandaa.
Jiandae na mwaka mpya unaokaribia kuanza.
Heri ya Krismasi, Hata Kama Mwaka Huu Imekuja Ghafla!
Heri ya Krismasi, Hata Kama Mwaka Huu Imekuja Ghafla!
Maggid Mjengwa,
Iringa.(P.T)
Iringa.(P.T)
0 comments:
Post a Comment