Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amekabidhiwa visima Vitatu vyenye thamani ya Shilingi Milioni 48.5 toka kwa Shirika lisilo la kiserikali toka Nchini Omani linaitwa kwa TUELEKEZANE PEPONI chini ya Afisa Mtendaji wake Nasr Al Jahdhamy.
Akizungumza wakati wa kukabidhi visima hivyo Mbunge huyo alisema kuwa , shida ya maji ndani ya Halmashauri ya chalinze imekuwa kubwa na kueleza kuwa kazi iliyofanyika kufanikisha ujenzi wa visima hivyo ni kubwa ili kusaidia tatizo hilo kwa kipindi hiki wakati wakisubiri kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa kutoa maji mto wami.
"Nimeona nifanye kazi ya kutengeneza visima ili kupunguza ukali wa uhaba wa maji kwani matengenezo ya mradi wa wami bado yanaendelea kuchimbwa kwa visima hivi si ishara kuwa ule mradi wa maji ambao tuliongea kuwa umekufa mradi wa wami utakapokamilika tunataraji utawanufaisha wananchi wengi wa jimbo letu."alisema Ridhiwani
Aidha visima hivyo vitatu vimekabidhiwa katika kijiji cha matipwili , shule ya sekondari ya matipwili na kijiji cha Gongo ambavyo vinaendelea kujengwa na vinataraji kukamilika mapema ndani ya wiki ijayo.
Naye Bwana Naseer aliahidi kuendelea kumsaidia Mbunge kufikia malengo yake ya kusaidia kutatua changamoto zinazokabili nyimbo hilo,na kuongeza kuwa atasaidia kuchimba visima vingine kumi katika Halmashauri hiyo na kusaidia michezo.
0 comments:
Post a Comment