Afisa wa Mradi wa IIDEA, Bi. Angela Kilusungu wa CDEA, akisoma taarifa fupi juu ya mradi huo mpya wa utakaosaidia sanaa kwa Afrika Mashariki
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya CDEA, wakiwa katika mkutano huo
Allen Enjewele wa CDEA akifanya mahojiano katika tukio hilo
Msanii Remigius Sostenes wa CDEA akitoa burudani katika tukio hilo
Mwenyekiti wa Bodi wa CDEA, Mzee Madaraka Nyerere akijadiliana jambo na Mjumbe wa bodi hiyo ambaye anatokea Burundi, Bw. Gilbert Hagabimana wakati wa uzinduzo huo.
Baadhi ya wadau wa Sanaa nchini wakijadiliana katika uzinduzi huo
Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bi. Ayeta Anne Wangusa (kushoto) akijadiliana jambo na wadau wa sanaa
Msanii Nick wa Pili akielezea namna sanaa inavyohitaji ubunifu wakati wa tukio hilo
Baadhi ya wadau wa sanaa na wanahabari wakipata kujadiliana jambo
Wadau wa sanaa wakifuatilia makala fupi ya CDEA iliyokuwa maalum wakati wa uzinduzi huo
Uzinduzi huo ukiendelea
Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bi. Ayeta Anne Wangusa akielezea jambo katika tukio hilo
Mwenyekiti wa Bodi wa CDEA, Mzee Madaraka Nyerere akitoa neno na kumkaribisha mgeni rasmi
Mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa Bw.Habibu Msammy aliyemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizindua rasmi mradi huo
Mzee Kitime mmoja wa wadau wa Sanaa nchini akifuatilia kwa makini tukio hilo la uzinduzi
Wadau wa kifuatilia uzinduzi huo
Wajumbe wa Bodi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya uzinduzi wa mradi huo wa IIDEA, mapema leo Novemba 25.2016.
PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE
SHIRIKA
lisilo la kiserikali la Culture and Development East Africa (CDEA) leo
limezindua rasmi mradi wa Atamishi ya kazi za sanaa (IIDEA) ambapo
utakuwa nguzo muhimu kwa nchi za Umoja Wa Afrika Mashariki ikiwemo
Tanzania na Uganda.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa Bw.Habibu
Msammy aliyemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mh. Nape Nnauye, ameeleza kuwa sanaa ni ajira hivyo mpango huo utasaidia
kuinua ajira kwa wasanii watakaofikiwa na kukuza soko la Afrika
Mashariki kupitia Sanaa zao.
“Sanaa
ni kazi ya kujikimu na kazi ni hutu hivyo ni wajibu wa kila msanii
kujiheshimu na kufuata taratibu ili kuwa njia kwa jamii na kuheshimika
zaidi hasa katika sanaa yake. Nawapongeza sana CDEA kwa mpango huu kwani
utaendelea kudumisha umoja wa Afrika Mashariki, utasaidia Wasanii wetu
kupanua mawazo yao zaidi na kujiongezea maarifa ya juu katika taaluma
yao ya Sanaa.” Alieleza Bw. Habibu Msammy.
Pia
alisisitiza kuwa mafunzo watakayoyapata wayatumie kujiimalisha kiuchumi
huku akisisitiza kuwa bado wanayo nafasi ya kujifunza zaidi katika
kuweza kubuni vazi la Taifa.
“Kwa
kuwa mradi huu unagusa sanaa za Ubunifu wa mavazi, Urembo na filamu.
Wabunifu wa Tanzania ni wasaha wa kuendelea kubuni vazi la Taifa,
Wasanii wanaangaliwa na wengi hivyo kuanzia mavazi na mawazo yao ya
ubunifu na tunawategemea pia katika kubuni vazi letu la Taifa” alieleza
Habibu Msammy.
Mradi huo wa mwaka mmoja unatarajia kuanza kutoa mafunzo kwa wabunifu wa mavazi na urembo, Wanamuziki na wasanii wa filamu.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bi. Ayeta Anne Wangusa
amebainisha kuwa, baada ya mwezi mmoja kuanzia sasa wataanza mchakato
wa kupata washiriki ambapo wahusika watatakiwa kutuma maombi ya ushiriki
baada ya kuona matangazo mbalimbali yatakayotolewa na CDEA kupitia
mitandao ya kijamii na sehemu zingine za Utamaduni.
Katika
uzinduzi huo, watu mbalimbali wameshiriki wakiwemo wasanii wa filamu,
maigizo, wabunifu wa mavazi, wanahabari, wanamuziki na wasanii wa kazi
za sanaa ikiwemo za mikono na ubunifu.
0 comments:
Post a Comment