Na Woinde Shizza,ArushaWito umetolewa kwa jamii ili waweze kuwa na maisha bora wawe na shughuli za halali za kufanya zitakazo waingizia kipato,ili wasiwe tegemezi katika familia zao na jamii kwa ujumla.
Kauli
hiyo imetolewa na Jaggy Singh ambaye ni mkurugenzi mkuu wa ushirika wa
Kimataifa wa wafanyabiashara Wakristo ( FGBMFI),ambapo amewataka watu
kufanya shughuli zao katika misingi iliyo halali ,katika uadilifu na
waepuke udanganyifu.
Singh
amesisitiza kuwa lengo kuu la mkutano ni kuwaleta wafanyabiashara pamoja
kubadilishana mawazo na changamoto wanazopitia,kuonyesha umuhimu wa
kuishi maisha ya uhalisia na kufanya kazi kwa bidii zaidi,ambapo
amewataka kuepuka udanganyifu wasiipige serikali chenga kwa kutokulipa
kodi ,wafuate utaratibu na sheria za nchi.
Kwa
upande wake raisi wa (FGBMFI) nchini Tanzania Injinia John Njau amesema
ushirika huo wa wafanyabiashara wa Kimataifa hawajishughulishi na
biashara peke yake bali wanahubiri Injili kamili kwa kutoa ushuhuda wa
vitendo hata kama wafanyabiashara wengine hawaamini lakini wao
wanatimiza wajibu.
Ameainisha kuwa nchini Tanzania kwa sasa wana matawi ya ushirika huo wa wafanyabiashara Wakristo yapatayo(7) ambayo ni kama ifuatavyo,
Mbeya,Mwaza,Shinyanga,Kilimanjaro,Arusha,Dar
es-salaam,Manyara pamoja na Zanzibar ,na kwa upande wa Kimataifa kwa
ujumla yapo 169,ambapo kila tawi linafanya kazi kutokana na taaluma
walizo nazo.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo John Majo
,ambaye pia ni mwenyekiti wa tawi la Arusha ,amesema kuwa ushirika huo
wa wafanyabiashara wa Kikristo mtu yeyote anaruhusiwa kujiunga maadamu
anajishughulisha ,awe ameajiriwa ,mfanyabiashara ,au mjasiriamali
anaruhusiwa nia yao kuu ni kuwaleta pamoja ili wamjue Mungu zaidi pia
Aidha
amewataka vijana wa kiume wasipende maisha ya urahisi bali wachape kazi
kwa bidii,wajitume waache tabia mbaya ya kuwa tegemezi kwani wananguvu
Mungu amewapa wazitumie ili kujiingizia kipato kwani itawajengea heshima
katika jamii
“Unamkuta
kijana yupo tu mtaani hataki kujishughulisha ukimtazama hana ulemavu
wowote ,anapenda maisha ya kifahari na starehe lakini kazi hataki
kufanya matokeo yake anajikuta amejiingiza kwenye mambo ya aibu na
fedheha kubwa katika jamiii,inatuhuzunisha sana sisi kama wazazi
badilikeni mjitume “alisisitiza John.
0 comments:
Post a Comment