Na Masanja Mabula -Pemba
MKUU wa
Mkoa wa Kaskazini Pemba , Omar Khamis Othman amewashauri walimu Wakuu wa
Skuli za Wilaya ya Micheweni kuanzisha English Club na English Class
ili kuwajengea uwezo wanafunzi ya kujiajiri kupitia sekta ya kitalii
mara baada ya kumaliza masomo yao.
Amesema
ni vyema walimu hao hususani wanaotoka maeneo ya uwezekaji kuzitumia
fursa zilizopo kwa kuwajengea uwezo wa wanafunzi wa kujua kuongea na
kuandika kwa ufasaha lugha ya kiingreza ili kuwafanya wanufaike na uwepo
wa sekta ya utalii katika maeneo yao .
Akizungumza
na walimu Wakuu wa Skuli za Msingi na Sekondari Wilayani hapa kwenye
ukumbi wa chuo cha walimu Wingwi , Mkuu huyo ameeleza kufurahishwa na
hatua iliyofikiwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu Zanzibar (ZEDO)
kuanzisha English Club pamoja na English Class kwa baadhi ya Skuli za
Zanzibar .
Amefahamisha
kuwa uwamuzi wa kuanzishwa English Club pia kutasaidia kuongeza ufaulu
wa wanafunzi katika mitihani yao ya Taifa kwani watakuwa na uwezo ya
kujibu vyema mitihani kwa umakini .
“Zipo
fursa nyingi ambazo zinaweza kuwasaidia vijana kuweza kujiairi wenyewe
kupitia sekta ya utalii ikiwa wataandaliwa vyema na kujengewa msingi ya
kuweza kuongea na kuandika kwa ufasha lugha ya kiingreza “alisema .
Mapema
akizungumza kwenye mkutano huo , Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya
Elimu Zanzibar (ZEDO) Ussi Said Suleiman amesema kwamba Jumuiya hiyo
imekuwa ikitoa mbinu bora za upasishaji wa wanafunzi kupitia sekta ya
michezo na sanaa.
Amesema
ni vyema walimu wakawa wabunifu wa kubuni mbinu ambazo zitawavutia
wanafunzi na kuwafanya wasome kwa ushindani ikiwemo njia ya michezo na
sanaa pamoja na kuanzisha englis club na english class katika skuli zao .
“Ni
lazima walimu kubuni mbinu bora za upasishaji wanafunzi katika mitihani
yao ya Taifa ambapo suala la michezo na sanaa linaweza kusaidia kufikiwa
kwa lengo la kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya Taifa
“alifahamisha.
Aidha
aliwataka walimu wakuu kuwashajihisha wanafunzi ambao hawatapata fursa
ya kuchaguliwa kuendelea na masomo , kujiunga na chuo cha Ufundi Dodoeni
ambacho kinatoa mafunzo ya ufundi na ujasiriamali lengo n kubakabiliana
na tatizo la ajira kwa vijana wanaomaliza masomo yao .
0 comments:
Post a Comment