Thursday, October 20, 2016

MKUU WA MKOA KASKAZINI PEMBA ASHAURI WALIMU KUANZISHA KLABU ZA LUGHA YA KIINGEREZA



Na Masanja Mabula -Pemba

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba , Omar Khamis Othman amewashauri walimu Wakuu wa Skuli za Wilaya ya Micheweni kuanzisha English Club na English Class ili kuwajengea uwezo wanafunzi ya kujiajiri kupitia sekta ya kitalii mara baada ya kumaliza masomo yao.

Amesema ni vyema walimu hao hususani wanaotoka maeneo ya uwezekaji kuzitumia fursa zilizopo kwa kuwajengea uwezo wa wanafunzi wa kujua kuongea na kuandika kwa ufasaha lugha ya kiingreza ili kuwafanya wanufaike na uwepo wa sekta ya utalii katika maeneo yao .

Akizungumza na walimu Wakuu wa Skuli za Msingi na Sekondari Wilayani hapa kwenye ukumbi wa chuo cha walimu Wingwi , Mkuu huyo ameeleza kufurahishwa na hatua iliyofikiwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu Zanzibar (ZEDO) kuanzisha English Club pamoja na English Class kwa baadhi ya Skuli za Zanzibar .

Amefahamisha kuwa uwamuzi wa kuanzishwa English Club pia kutasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika mitihani yao ya Taifa kwani watakuwa na uwezo ya kujibu vyema mitihani kwa umakini .

“Zipo fursa nyingi ambazo zinaweza kuwasaidia vijana kuweza kujiairi wenyewe kupitia sekta ya utalii ikiwa wataandaliwa vyema na kujengewa msingi ya kuweza kuongea na kuandika kwa ufasha lugha ya kiingreza “alisema .

Mapema akizungumza kwenye mkutano huo , Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu Zanzibar (ZEDO) Ussi Said Suleiman amesema kwamba Jumuiya hiyo imekuwa ikitoa mbinu bora za upasishaji wa wanafunzi kupitia sekta ya michezo na sanaa.

Amesema ni vyema walimu wakawa wabunifu wa kubuni mbinu ambazo zitawavutia wanafunzi na kuwafanya wasome kwa ushindani ikiwemo njia ya michezo na sanaa pamoja na kuanzisha englis club na english class katika skuli zao .

“Ni lazima walimu kubuni mbinu bora za upasishaji wanafunzi katika mitihani yao ya Taifa ambapo suala la michezo na sanaa linaweza kusaidia kufikiwa kwa lengo la kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya Taifa “alifahamisha.

Aidha aliwataka walimu wakuu kuwashajihisha wanafunzi ambao hawatapata fursa ya kuchaguliwa kuendelea na masomo , kujiunga na chuo cha Ufundi Dodoeni ambacho kinatoa mafunzo ya ufundi na ujasiriamali lengo n kubakabiliana na tatizo la ajira kwa vijana wanaomaliza masomo yao .

Amesema kupitia mbinu hiyo wameweza kuwarudisha Skuli wanafunzi waliokuwa wameacha masomo kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ukosefu wa vifaa na sare .

No comments:

Post a Comment