Afisa
Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Mkoa wa Mwanza Bw. Daud
Hashimu Abdallah akiwasilisha taarifa ya usajili wa watumishi wa umma
kwa ajili ya kupatiwa Vitambulisho vya Taifa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J.
Kairuki (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo
mkoani Mwanza kwa ajili ya kukagua na kufanya tathmini ya zoezi la
usajili wa watumishi wa umma ili kupata Vitambulisho vya Taifa.
Mkurugenzi
wa Halimashauri ya Wilaya Misungwi Bw. Eliurd L. Mwaiteleke (kulia)
akimuongoza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (katikati) kwenda katika
moja ya kituo cha kusajili watumishi wa umma kwa ajili ya kupatiwa
Vitambulisho vya Taifa wakati wa ziara ya waziri huyo ili kuona namna
zoezi hilo linavyoendeshwa katika Halimashauri ya Wilaya Misungwi.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angellah J. Kairuki akipewa ufafanuzi na Afisa Usajili wa Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa wa Halimashauri ya Wilaya Misungwi Bw. Abbasi
Iwodya (kulia) juu ya taarifa zinazowasilishwa na watumishi wa umma kwa
ajili ya kupatiwa Vitambulisho vya Taifa wakati wa ziara ya kikazi ya
waziri huyo aliyoifanya katika Halimashauri ya Wilaya Misungwi.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na mmoja wa watumishi
aliyekuwa akijisajili kwa ajili ya kupata Kitambulisho cha Taifa
wakati wa ziara ya waziri huyo ya kukagua na kufanya tathmini ya zoezi
hilo katika Halimashauri ya Wilaya Misungwi.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akikagua viambatanisho vya malalamiko
yaliyowasilishwa na mmoja wa watumishi wa Halimashauri ya Wilaya
Misungwi wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo aliyoifanya katika
Halimashauri hiyo ili kukagua na kufanya tathmini ya zoezi la usajili wa
watumishi wa umma kwa ajili ya kupatiwa Vitambulisho vya Taifa mkoani
Mwanza.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akipokea malalamiko ya mtumishi wa
Halimashauri ya Wilaya Misungwi wakati wa ziara ya kikazi ya waziri
huyo aliyoifanya katika Halimashauri hiyo ili kukagua na kufanya
tathmini ya zoezi la usajili wa watumishi wa umma kwa ajili ya kupatiwa
Vitambulisho vya Taifa mkoani Mwanza.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Halimashauri
ya Wilaya Misungwi wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo
aliyoifanya katika Halimashauri hiyo ili kukagua na kufanya tathmini ya
zoezi la usajili wa watumishi wa umma kwa ajili ya kupatiwa
Vitambulisho vya Taifa mkoani Mwanza.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akishuhudia mtumishi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Ilemela akisajiliwa kwa ajili ya kupata Kitambulisho cha
Taifa wakati wa ziara ya waziri huyo ya kukagua na kufanya tathmini ya
zoezi hilo katika Halimashauri hiyo.
Baadhi ya
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana waliojitokeza kwa ajili
ya kujisajili ili kupata Vitambulisho vya Taifa wakimsikiliza Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi
ya waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri hiyo ili kukagua na
kufanya tathmini ya zoezi hilo.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akishuhudia usajili wa watumishi wa umma
wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana kwa ajili ya kupata Vitambulisho
vya Taifa wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo aliyoifanya katika
Halmashauri hiyo ili kukagua na kufanya tathmini ya zoezi hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisisitiza juu ya ukamilishaji wa zoezi la usajili wa watumishi wa umma mkoani Mwanza wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo mkoani humo, aliyoifanya kwa lengo la kufanya tathmini ya zoezi hilo . Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella akimsikiliza.
0 comments:
Post a Comment