Mshindi
wa Kwanza wea Division A wa Mashindano ya Wazi ya Arusha Open Kapten
Shaban Kibuna akiwa katika harakati za mchezo huo katika mashindano
yaliyomalizika Jumapili Oktoba 16 Jijini Arusha .(Picha na Luteni
Selemani Semunyu).
Mshindi
wa Kwanza wa kundi la Wadogo Junior wa Mashindano ya Wazi ya Arusha
Open Almadious Simon akiwa katika harakati za mchezo huo katika
mashindano yaliyomalizika Jumapili Oktoba 16 Jijini Arusha .(Picha na
Luteni Selemani Semunyu).
Mchezaji
wa Golf wa Timu ya JWTZ ya Lugalo Nicholous Chitanda akiwa katika
harakati za Mashindano ya Wazi ya Arusha Open katika mashindano
yaliyomalizika Jumapili Oktoba 16 Jijini Arusha .(Picha na Luteni
Selemani Semunyu).
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Mashindano ya Wazi ya Golf Arusha open yamemalizika jijini Arusha Oktoba 16 huku Timu ya Golf
ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo ikifanya vizuri
kwa kunyakua ushindi katika makundi kwa asilimia 53 huku ushindi wa
Jumla ukichukuliwa na Mchezaji kutoka klabu ya Kilimanjaro.
Mpiga
golf wa Timu ya Kilimanjaro issack Wanyeche akiibuka mshindi wa jumla
wa mashindano hayo yaliyokuwa yakishindanishwa kwa mtindo wa Mikwaju ya
Jumla Net kwenye makundi na Gross kwa ushindi wa Jumla.
Katika Division A Mshindi
ni kapteni Shaaban Kibuna kutoka Klabu ya Liugalo akifuatiwa na Richard
Mtweve naye wa Lugalo ambaye walifungana kwa Mikwaju ya Jumla 145 kila
mmoja lakini kutokana na kapteni kibuna kucheza vizuri siku ya mwisho
akamshinda Mtweve kutokana na kucheza net ya 70 kwa 75 wakatik siku ya
kwanza ilikuwa 75 kwa 70 ya Mtweve.
Kundi B ambalo Timu ya Lugalo haikuingiza mchezaji katika kundi hilol imechukuliwa na N Matsouka wa Arusha aliyepata mikwaju ya Jumla 143 akifuatiwa na mshindi wa pili ni Musadiq Versi aliyepiga mikwaju ya Jumla 147.
Divisheni C Mshindi
ni Talib Chagani aliyepiga Mikwaju ya Jumla 148 akifuatiwa na kapteni
Amanzi Mandengule wa lugalo aliyepiga mikwaju ya jumla 149.
Kwa upande wa Kundi la wadogo Junior mshindi ni Almadiuos Simon kutoka Klabu ya Jeshi ya Lugalo kwa kupiga Mikwaju ya Jumla 131 huku mshindi wa Siku ya kwanza ni Salim Sharifaliyepata Net ya 70 na Mshindi wa Siku ya Pili ni Clemence Mutavangu wa Lugalo aliyepiga Net ya 69.
Kwa Upande wake Nahodha wa Klabu ya jeshi ya Lugalo ambaye ni Mshindi wa Divisheni
A kapten Shaban Kibuna amesema wamefanya vizuri kutokana kuingiza
wachezaji 14 na kunyakua nafasi tano ukilinganisha na Arusha waliongiza
wachezaji zaidi ya 50 na TPC walioingiza wachezaji 17 na kutoka bila
ushindi.
Alisema
kinachofuata sasa ni klabu yake kujiandaa na mashindano yaliyoko mbele
yao ya Oktoba 22 Mwaka huu lakini pia wanatarajiwa kuwa na mshindano ya
Waitara Trophy na Miaka 10 ya Klabu mwezi Desemba.
0 comments:
Post a Comment