Makao makuu ya ICC, Hague, Uholanzi
Baadhi ya
nchi za Afrika zimeanza kujiondoa katika uanachama wa Mahakam ya
Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC). Siku nne baada ya rais wa Burundi
kusaini sheria ya kuindoa nchi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya
Uhalifu wa Kivita, Afrika Kusini imeanzisha mchakato wa kujiondoa kutoka
uanachama wa mahakama hiyo.
Afrika
kusini imechukua uamuzi wa kuanzisha mchakato huo kufuatia shinikizo
ilikumbana nazo mwaka uliopita kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu
wa Kivita za kuitaka imkamate rais wa Sudan Omar al Bashir wakati wa
mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Johannesburg.
Chini ya
pigo la ombi la kusafirishwa, Rais wa Sudan Omar al-Bashir (katikati)
amepiga picha ya pamoja na viongozi wa AU, Jumapili Juni 14.
Septemba
mwaka jana, Mahakama Kuu ya Afrika Kusini iliinyima serikali ya nchi
hiyo ruhusa ya kukata rufaa uamuzi ulioishutumu kwa kukosa kumkamata
Omar al Bashir aliposhiriki mkutano huo mwezi Juni mwaka 2015.
Serikali
ilijaribu kukata rufaa uamuzi wa Mahakama Kuu ikisema Bashir alikuwa na
kinga ya urais kwa sababu yeye ni kiongozi wa taifa.
Lakini Jaji Hans Fabricius alisema rufaa hiyo haiwezi kufanikisha chochote.
“Afrika
Kusini ni mwanachama wa Mkataba wa Roma uliounda Mahakama ya Kimataifa
ya Uhalifu wa Kivita, na mkataba huo unabatilisha sheria zote ambazo
huenda zingempa kinga Bashir asikamatwe na kushtakiwa”, amesema Jaji
Hans Fabricius.
Kiongozi
huyo wa Sudan amekuwa akisakwa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa
kivita ICC kwa tuhuma za kutekeleza mauaji ya halaiki na makosa ya
uhalifu wa kivita Darfur.
Omar ala
Bashiri aliyechukua mamlaka kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989
amekuwa akisakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) kwa
tuhuma za kutekeleza mauaji ya halaiki na makosa ya uhalifu wa kivita
katika jimbo la Darfur, madai ambayo Bw Bashiri amekanusha.
Itafahamika kwamba nchi nyingi za Afrika zinailaumu ICC kwa kuzilenga zaidi nchi za Afrika.RFI
0 comments:
Post a Comment