Mwezi mmoja tangu Serikali iseme usalama wa chakula ni kwa asilimia 123, jana Ofisi ya Waziri Mkuu imezitaka wizara, mikoa na halmashauri kuchukua hatua za kukabiliana na tishio la njaa ikiwamo kuzuia matumizi ya nafaka kutengeneza pombe.
Pia,
ofisi hiyo ya Waziri Mkuu imewataka wananchi kuhifadhi chakula baada ya
Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), kutabiri kuwa kuanzia Oktoba hadi
Desemba mwaka huu, maeneo mengi ya nchi yatakuwa na mvua zitakazonyesha
chini ya kiwango huku maeneo mengine yakikumbwa na ukame.
Akizungumza
jana, Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia
Mbaazi Msuya alisema hali hiyo itasababisha ukame na tishio la njaa
katika baadhi ya maeneo ambayo hutegemea mvua katika kilimo.
Msuya
alisema kutokana na utabiri wa TMA, wananchi wanashauriwa kulima mazao
ya muda mfupi na yanayostahimili ukame.
“Maofisa ugani wanatakiwa kutoa
ushauri kwa wananchi kuhusu mazao wanayotakiwa kupanda kwenye maeneo
yao,” alisema.
Aliwataka wananchi kuweka akiba ya chakula cha kutosha
hasa kwenye maeneo ambayo yanapata mvua chini ya kiwango.
Kaimu
Mkurugenzi, Idara ya Usalama wa Chakula wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na
Uvuvi, MaryStela Mtalo alisema idara hiyo itafanya kazi ya uratibu,
ufuatiliaji na ukusanyaji na kutoa taarifa za chakula kwa wakati.
“Wakala wa Taifa Hifadhi ya Chakula wanaelekezwa kununua na kuhifadhi
akiba ya chakula cha kutosha ili kukabiliana na upungufu unaotarajiwa
katika baadhi ya maeneo,” alisema.
“Mikoa na Halmashauri zake zisimamie
na kuimarisha mifumo ya kuhifadhi chakula baada ya mavuno ili kupunguza
upotevu wa chakula na kuhakikisha chakula kinapatikana.”
Taarifa hii ya
tishio la njaa inapingana na ile iliyotolewa Septemba 8 na Naibu
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Tate Ole Nasha kwamba
Watanzania wasiwe na wasiwasi kuhusu hali ya chakula nchini kwa maelezo
kuwa kuna ziada ya chakula zaidi ya asilimia 123 ikilichozalishwa msimu
uliopita.
Akizindua tovuti ya Wakala wa Taifa Hifadhi ya Chakula (NFRA)
mjini Dodoma, Naibu Waziri Ole Nasha alisema hali ya chakula inaridhisha
kutokana na ukweli kuwa uzalishaji wa chakula ni kwa asilimia 100 hali
ya utoshelevu wa chakula ni asilimia 101 hadi 120 hali inayotafsiriwa
kuwa kuna chakula cha kutosha kwa miaka mitatu hadi minne.
“Nawasihi
Watanzania kutunza chakula kilichopo ili kitumike sasa na baadaye,
hali ya uwepo wa chakula
ndani ya nchi itaonyesha kuwa kuna usalama kwa wananchi na wanaweza
kuendelea na shughuli zao za kila siku,” alisema.
Pia ni
tofauti na taarifa iliyotolewa Jumanne iliyopita na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Kilimo, Chakula na Mifugo Dk Florence Turuka kwamba wilaya 42
nchini zinakabiliwa na uhaba wa chakula huku Mkoa wa Kagera ukikumbwa na
baa la njaa na ukame.
Kutokana na ukame huo, ng’ombe waliokuwa wanauzwa kwa Sh 600,000 wilayani Karagwe sasa wanauzwa kwa Sh 20,000.
Kutokana na ukame huo, ng’ombe waliokuwa wanauzwa kwa Sh 600,000 wilayani Karagwe sasa wanauzwa kwa Sh 20,000.
“Licha ya
kwamba ripoti ya dunia inaonyesha hali ya chakula duniani ni mbaya,
Tanzania kipo chakula na kinatosheleza kwa kiwango cha juu cha asilimia
123,”alisema Turuka wakati akizindua ripoti ya Shirika la Chakula na
Kilimo Duniani (FAO) kwa mwaka 2016 inayoonyesha kuwa dunia inakabiliwa
na balaa la njaa kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
0 comments:
Post a Comment