
Mh. Nuhu Mwamwindi akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwembetogwa, Bi Monica Kafumu mifuko ya saruji.
Msaada huo aliutoa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Matron wa Shule hiyo
Mbunge wa
Viti maalum atokanaye na Jumuiya ya WAZAZI( C.C.M) Tanzania Bara, Mh.
Zainab Nuhu Mwamwindi amesema kuwa jamii inahitaji kuhamasishwa na
kukumbushwa wajibu muhimu wa kuunga mkono masuala muhimu yakiwemo yale
yanayoweza kusaidia kusukuma mbele jamii ikiwemo elimu.
Aidha kwa
kuguswa na mchango muhimu unaotolewa na walimu wa shule hiyo, Mh. Nuhu
Mwamwindi alichangia papo hapo shilingi laki moja kwa ajili ya chai ya
walimu shuleni hapo.

Mh.Mwamwindi akikagua mabweni ya hosteli ya wasichana iliyopo shuleni hapo.

0 comments:
Post a Comment