METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, April 30, 2020

BASHUNGWA AWAPONGEZA MUHIMBILI KWA KUTENGENEZA VAZI MAALUMU LA WAUGUZI




Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akiwa amevaa  vazi maalum (coverall) la wauguzi lilotengenezwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ameupongeza uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kutengeneza mavazi maalum (coverall) za wauguzi ambayo yanasaidia wahudumu wa afya kujikinga na ugonjwa wa Corona.

“Nawapongeza hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kutengeneza mavazi maalum (coverall) ya wauguzi Mungu awabariki na kuwalinda wauguzi wetu”.

Aidha, amevipongeza viwanda vyote nchini kwa kuendelea kuhakikisha vinatoa mchango mkubwa kwa kipindi hiki cha kupambana na ugojwa wa Corona na ametoa wito kwa viwanda na mtanzania yeyote anaeweza kutengeneza mavazi maalum ya wauguzi ajitokeze na awasiliane na Wizara ya Viwanda na Biashara.

“Viwanda vyetu nchini hamjawahi kuniangusha, yeyote anayeweza kutengeneza awasiliane na Wizara ya Viwanda na Biashara namba ya simu +255784218155"  ili kupata muongozo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com