Jeshi la
Congo limesema Jumapili (14.08.2016) kwamba takriban raia 36 wameuwawa
katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambalo
limekumbwa na matumizi ya nguvu tokea mwaka 2014.
Msemaji
wa jeshi Mak Hazukay ameliambia shirika la habari la AFP kwamba
watuhumiwa waasi wa kundi la Allied Demokratic Forces (AFD) ambalo ni
kundi la Waislamu wa itikadi kali wenye asili yao nchini Uganda
limeuwawa "watu 36" katika mji wa Beni Jumamosi usiku.
Amesema
"ndio kwanza wamegunduwa miili yao."katika kitongoji cha Rwangoma kwenye
viunga vya mji wa Beni na kwamba miili zaidi inaendelea kutafutwa.
Kwa
mujibu wa msemaji huyo wa jeshi waasi hao wa ADF wameweza kukwepa maeneo
waliyoko majeshi ya serikali na kuweza kuingia katika maeneo walioko
raia na kuwauwa katika kulipiza kisasi kwa jili ya operesheni za kijeshi
zinazofanyika katika eneo hilo.
Gilbert
Kambale kiongozi wa shirika la kiraia katika eneo hilo amesema shambulio
hilo limetokea kati ya saa moja usiku na saa tano za usiku hapo
Jumamosi na kwamba tayari kulikuwa na miili 35 katika chumba cha
kuhifadhia maiti katika hospitali ya Beni.
Kambale
amesema kuna hasira kubwa sana kutokana na kushindwa kwa serikali
kurudisha usalama katika eneo hilo na kwamba inatia wasi wasi kutokana
na kwamba rais wa jamhuri alikuwako katika eneo hilo na halafu yanakuja
mauaji hayo.
Beni yaathirika zaidi
Mauaji
hayo mapya yamepelekea maandamano makubwa yaliyojaa ghadhabu ambapo watu
wanaofikia mia moja wametoka mitaani na kauli mbiu za kuipinga serikali
na kudai usalama.
Mauaji
hayo yametokea siku tatu baada ya Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya
kidemokrasi ya Congo kuutembelea mkoa huo na kuahidi kufanya kila
awezalo kuleta amani na usalama katika eneo hilo.
Beni iko
katika Mkoa wa Kivu Kaskazini jimbo ambalo limeshuhudia mfululizo wa
mashambulizi ambayo serikali na Umoja wa Mataifa inalialumu kundi hilo
la ADF kwa kuhusika nayo.
Hususan
eneo la Beni limekuwa likishuhudia mauaji kadhaa tokea mwaka 2014 ambayo
kwa jumla yamepelekea zaidi ya raia 600 kupoteza maisha yao.
Mauaji yazusha maandamano
Wakati wa
mchana takriban waandamanaji 100 waliokuwa wameubeba mwili wa mmojawapo
wa wahanga walikusanyika mjini wakipiga mayowe ya ghadhabu dhidi ya
Kabila na serikali yake.
Mwanaharakati
wa haki za binaadamu katika eneo hilo Jackson Kesereka amesema wakaazi
kaskazini mwa mji huo walikuwa wakiunguza matairi barabarani kupinga
mauaji hayo na kuonyesha hasira yao kwa serikali.
Kwanza
wakaazi wa eneo hilo waliwadhania waasi hao kuwa ni wanajeshi kabla ya
kuanza kushambuliwa kwa mapanga na kupigwa risasi.Shambulio hilo
linasemekana kuwa la kikatili kabisa kuwahi kufanywa na waasi wa ADF
mwaka huu.
Hivi
karibuni Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo alikutana
na kiongozi mwenzake wa Uganda,Yoweri Museveni na kuzungumzia
ushirikiano katika mapambano dhidi ya waasi wa ADF ambao wanampinga Rais
Museveni na wamekuwepo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
kwa zaidi miaka 20.
DW
0 comments:
Post a Comment