Wawakilishi
pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Yanga SC, wametupwa nje
kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, baada ya TP
Mazembe kuchapwa mabao 3-2 na Medeama ya Ghana katika mchezo wa kundi A
uliofanyika kunako dimba la Essipong huko Sports Takoradi, Ghana.
Medeama
walipata mabao yao kupitia kwa Enock Atta Agyei, Moses Amponsah Sarpong
na Kwesi Donsu huku Mazembe wakipata mabao yao yote mawili kupitia kwa
Jonathan Bolingi.
Kufuatia
matokeo hayo, Medeama ambao mchezo wa mwisho watacheza na MO Bejaia ya
watahitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu hatua ya nusu fainali, wakati
huo Yanga watakuwa ugenini wakikipa na TP Mazembe mjini Lubumbashi,
mchezo ambao utakuwa ni wa kukamilisha ratiba tu kwa upande wa Yanga.
CHANZO- http://www.barakampenja.com
0 comments:
Post a Comment