METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 23, 2016

Brussels yakumbwa na mashambulizi ya kigaidi

Belgien Brüssel Flughafen Zaventem Passagiere Evakuierung
Kumetokea miripuko miwili katika uwanja wa ndege wa Zaventem mjini Brussels Ubelgiji na mwengine katika kituo cha treni cha Maelbeek kulichopo karibu na majengo ya taasisi za Umoja wa Ulaya.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini humo, hadi sasa idadi ya watu walioripotiwa kuwawa katika milipuko ya uwanja wa ndege wa Zaventem imefika 13 wengine 35 wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali. Usalama umeimarishwa katia uwanja wa ndege huwo. Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema walisikia sauti za risasi pamoja na watu wakipiga kelele kwa lugha ya kiarabau muda mfupi kabla ya kutokea milipuko hiyo.

Kwa upande mwengine kumekuwa na taarifa za kukinzana juu ya mripuko wa kituo cha treni, watu kumi wameripotiwa kuuwawa kwa mujibu wa shirika la utangazaji la VTM la Ubelgiji, lakini bila ya kutoa maelezo zaidi, huku vyanzo vyengine vikisema hamna aliyeathirka katika mlipuko huwo. Na Shirika la utangazaji wa Umma la VRT nchini humo limesema mlipuko wa uliotokea katika kituo cha reli ni wa kujitoa muhanga. Halikadhalika mamlaka ya usafiri ya Ubelgiji imesema usafiri wote wa umma mjini humo umesimamishwa ikiwamo wa reli na mabasi.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ubelgiji, Jan Jambon, ameitangaza nchi hiyo kuwa katika hali ya hatari ya kiwango cha nne ambacho ndio cha juu kabisa. Huku baraza la mawaziri nchini humo likiwa tayari limeitisha mkutano wa dharura mara tu baada ya kutokea kwa mashambulizi hayo.
Usalama waimarishwa nchi kadhaa za Ulaya

Halikadhalika serikali ya nchi hiyo inategemewa kukutana na waandishi habari kuyazungumzia mashambulizi hayo. Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel ameandika katika ukurasa wake wa Twitter, kuwa serikali inafuatilia kilahatua ya matukio hayo. Na kuongeza kwa sasa kipaumbele watapewa walioathirika na wale ambao wapo katika uwanja wa ndege huwo, eneo la mashambulizi.

Pamoja na hayo, nchi kadhaa za Ulaya zimeimarisha usalama katika viwanja vya ndege ikiwamo wa mjini Frankfurt hapa Ujerumani, Gatwick mjini London, Uingereza pamoja na Charles De Gaulle mjini Paris Ufaransa. Halikadhalika shirika la ndege la Aegean la Ugiriki limesitisha safari zake zote zinazoelekea mjini Brussels.

Na kwa upande wa Ufaransa rais wa nchi hiyo Francois Hollande ameitisha mkutano wa dharura na Waziri wake Mkuu, Waziri wa Ulinzi pamoja na Waziri wa mmabo ya ndani. Halikadhalika Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ameitisha mkutano na kamati ya dharura ya serikali nchini humo na kusema nchi hiyo itasaidia vyovyote iwezanvyo.

Miripuko hiyo inakuja siku chache baada ya kukamatwa kwa Salah Abdeslam mjini Brussels, mshukiwa mkuu wa mashambulizi ya mjini Paris mwezi Novemba mwaka jana ambapo watu 130 kuwawa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com