METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, June 4, 2015

WAKATI UTAZUNGUMZA

 

Na Mathias canal, Njombe

Pichani nipo Njombe hapa na Malisa Godlisten Mwenye flana nyekundu aliyewahi kuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi (SAUTSO) Chuo kikuu cha St Augustine mwaka 2012-2013 Sawia na mimi niliyewahi kuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala Dar es salaam City College (DACICOSTUA) 2013-2014. Pia Tupo na mtia nia ya Ubunge jimbo la Njombe Mjini kupitia CHADEMA Rose Mayemba ambaye ni Mtaalamu wa madawa aliyesoma (RUCO).

Tumejadili mengi sana juu ya uchaguzi mkuu nani ni nani mpaka sasa kwenye mchuano CCM kila mmoja hakuweka karata yake kwa yeyote yule wamesema wanadhani wanaendelea kusubiri watangaze nia zao wooote ndipo watasema nani ana hoja japo pia walisema kuna wagombea wananguvu ya pesa ila hawana nguvu ya hoja.

Wote wawili hawakusita kumzungumzia Edward Lowassa wanaamini CCM itakata jina lake na wanaamini Mbunge huyu wa Monduli atahamia ACT ngoja tuone hatma ya hili kwamba ni kweli maneno haya.Ila maoni yangu nakumbuka maneno ya Makongoro Nyerere wakati akitangaza nia anasema JK ana marafiki vibaka ila akiwashtukia tu anawamwaga.

Malisa yeye ni mtaalamu wa mawasiliano ya umma na mchambuzi wa maswala ya kisiasa sawa nami niliyebobea kwenye uandishi wa habari.

Kila lisemwalo ama hakika wakati utazungumza, NAAM Ni Neno La Wakati Mwema.

Mathias Canal
0756413465
Njombe-Tanzania
Share:

1 comment:

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com