METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, December 30, 2015

MCHUNNGAJI MSIGWA NA MEYA WAPATA KIBALI CHA KUWASHUKURU WAPIGA KURA WA IRINGA MJINI


MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na madiwani 14 wanaounda halmashauri ya manispaa ya Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kesho Desemba 31 watafanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Mwembetogwa mjini hapa kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa kuwapatia ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Katika mkutano huo, Mchungaji Msigwa, Mbunge wa Viti Maalumu Suzan Mgonakulima na Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe wataonesha muelekeo wa utekelezaji wa majukumu yao katika kipindi cha miaka mitano ijayo ili kuwaletea wananchi wa jimbo hilo maendeleo.

Mchungaji Msigwa anawaalika wananchi wote wa jimbo hilo, bila kujali itikadi zao kushiriki mkutano huo, na kuukaribisha mwaka mpya pamoja ili kusukuma gurudumu la maendeleo
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com