YANGA jana imerejesha furaha kwa mashabiki wake baada ya kushinda
mabao 3-0 dhidi ya Majimaji katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa kwenye
Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Mabingwa hao watetezi wa ligi hiyo wamepata ushindi jana baada ya
kutoka sare ya bila kufungana katika mechi dhidi ya Ndanda iliyochezwa
Mtwara, Jumatano ya wiki hii.
Yanga ilipata bao la kuongoza katika dakika ya 20, likifungwa na Deus
Kaseke aliyeuwahi mpira wa penalti iliyopigwa na Simon Msuva.
Awali, mwamuzi wa mechi hiyo Emmanuel Mwandebwa wa Arusha alitoa
penalti kwa Yanga baada ya mchezaji wa Majimaji kushika mpira eneo la
hatari na ndipo Msuva alipopiga penalti mara ya kwanza, lakini mwamuzi
alimtaka kurudia tena akidai alikosea, akaipiga mara ya pili ikaamuliwa
kurudia tena, akapiga mara ya tatu mpira ukagonga mwamba na ndipo Kaseke
alipouwahi na kuujaza wavuni.
Kipindi cha kwanza kiliisha kwa Yanga kuongoza kwa bao 1-0. Katika
kipindi hicho, Yanga walitengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa
kuzitumia huku Majimaji wakicheza kwa kuzuia zaidi. Amisi Tambwe
aliifungia Yanga bao la pili dakika ya 81 kwa kichwa, ikiwa ni baada ya
kufunga katika dakika ya 74 na mwamuzi kulikataa akidai mfungaji
aliotea.
Dakika tano baadaye, Tambwe aliongeza bao la tatu kwa pasi ya Juma
Mahadhi. Kutoka kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya, Azam jana iliendelea
kuzoa pointi kwenye uwanja huo baada ya kuifunga Mbeya City mabao 2-1.
Kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Ndanda ilitoka sare ya bila
kufungana na Kagera Sugar.
Huku kwenye uwanja wa Mwadui Shinyanga, Mwadui imetoka sare ya mabao
2-2 na Stand United. Katika uwanja wa Mabatini Mlandizi, Ruvu Shooting
iliitambia JKT Ruvu kwa kuifunga bao 1-0. Ligi hiyo inaendelea tena leo
kwenye uwanja wa Uhuru ambapo Simba itaikaribisha Mtibwa Sugar ya
Manungu, Turiani.
Mechi hiyo inatarajiwa kuwa kali na ya vuta nikuvute kutokana na timu
hizo kutambiana kwa zamu kila zinapokutana. Timu hizo zinakutana zikiwa
na makocha wapya Joseph Omog wa Simba na Salum Mayanga wa Mtibwa na
wote wakionesha kuwa wanalitaka taji kulingana na ubora wa vikosi vyao.
Mtibwa Sugar inapokutana na Simba au Yanga ni wazi kuwa hucheza kwa kukamia, lakini mwisho wa siku mmojawapo huibuka na ushindi.
Msimu uliopita timu hizi zilikutana raundi ya kwanza Januari 16,
mwaka huu Simba ikaibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa
kwenye Uwanja wa Taifa, pia ilipokutana katika raundi ya pili Mei 15,
mwaka huu bado Simba ilishinda bao 1-0.
Sunday, September 11, 2016
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. William Sam...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya akiangalia bamia zilizopandwa na Vijana wanaopata mafunzo katika kambi ya Mkongo leo tar...
-
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki zoezi la upandaji wa mbegu za pamba kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya mji wa Geita. Mkuu wa Mkoa wa Geita,akiwasili kwenye eneo la shamba na kusalimiana na viongozi wa halmashauri hiyo akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi.
Afisa Kilimo wa halmashauri ya mji,Bw Samwel Ng'wandu akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga.
Baadhi ya watumishi na Jeshi la akiba (MGAMBO)wakishiriki shughuli za kupanda mbegu kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya mji.
Wataalamu wa kilimo mkoani Geita wametakiwa kuwafuatilia kwa karibu wakulima wa pamba na kuwaelekeza kulima kwa tija ili kuzalisha zaidi tofauti na miaka ya nyuma.
Akizindua msimu wa kilimo cha pamba kwenye mashamba ya watumishi wa Halmashauri ya mji wa Geita yaliyoko kata ya Buhalahala ,Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema ni vema wataalam hao wakafika kwenye maeneo ya kilimo na kuwaelekeza wakulima kanuni zitakazowasaidia kuvuna pamba nyingi.
“Wito wangu kwa wakulima wote pamoja na wataalam wetu wa kilimo baada ya uzinduzi huu mkubwa kabisa wa kilimo cha pamba Mkoani kwetu,wataalam ni vyema wakawasaidia wakulima kufuata zile kanuni kumi bora za kilimo ambacho kitaweza kuwa saidia wakulima lakini nataka twende kisayansi zaidi”Alisema Luhumbi.
Mhandisi Luhumbi Aliongezea Kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kumsaidia mkulima na kuwataka wakulima kuchangamkia fursa hiyo na kuwekeza katika sekta ya kilimo cha pamba kwa kuwa hali ya hewa ya mwaka huu ni nzuri.
Mshahuri wa kilimo cha Mkataba Mkoani Geita Bw Joshua Mirumbe alisema lengo ni kuhakikisha wanaongeza tija ya uzalishaji kutoka wastani wa kilo 250 hadi 300 na kwenda kwa wastani wa kilo 800.
Katika msimu wa mwaka 2016/2017 mkoa wa Geita ulilenga kulima hekta 67002 zilizotarajiwa kuzalisha tani ,93437 za pamba lakini utekelezaji ulikuwa hekta 24 791 zilizozalisha tani 13 267.8 zenye thamani ya Sh Bilioni 15.Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki zoezi la upandaji wa mbegu za pamba kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya ... -
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment