METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, October 29, 2015

Wanaotaka tiketi ya Republican washambuliana

Republican
Trump alishutumiwa kwa mtazamo wake kuhusu wahamiaji
Wanaowania nafasi ya kuwania urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican walijibizana vikali kwenye mdhahalo wa tatu ulioandaliwa Colorado.
Donald Trump na Ben Carson, ambao hawana uzoefu mkubwa kisiasa lakini ndio wanaoongoza kinyang’anyiro hicho, walianza kushambuliwa tangu mwanzo wa mdahalo.
Gavana wa Ohio John Kasich alikashifu mpango wao “wa ndoto kuhusu ushuru” ana akaongeza kuwa: “Hatuwezi kumchagua mtu asiyeifahamu kazi.”
Bw Carson, ambaye ni daktari mstaafu, na ambaye amempita Bw Trump kwenye kura za maoni kitaifa, hakufana sana.
Pendekezo lake kuhusu ushuru, linalofuata mfumo wa zaka kwenye Biblia, ulishutumiwa vikali na Bw Kasich, ambaye pia alishutumu vikali mpango wa Bw Trump wa kufurusha wahamiaji 11 milioni kutoka Mexico na pia kujenga ukuta kwenye mpaka wa taifa hilo na Mexico.
Mdahalo huo haukujali urafiki wa kisiasa, kwani Gavana wa Florida Jeb Bush na Seneta wa Florida Marco Rubio pia walishambuliana.
Bw Bush alimhimiza Rubio, ambaye wakati mmoja alikuwa anajifunza siasa chini yake, kujiuzulu kutoka seneti kutokana na rekodi yake mbaya ya upigaji kura.
Wanahabari pia walishambuliwa, seneta wa Texas Ted Cruz akishangiliwa sana alipowashambulia waandalizi wa mdahalo huo CNBC kwa kuchochea uhasama.
"Maswali ambayo yameulizwa kwenye mjadala huu kufikia sasa yanayonyesha ni kwa nini raia huwa hawawaamini wanahabari," alisema.
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya chama cha Republican Reince Priebus pia alilalamikia maswali ya CNBC.
Upigaji kura wa kuamua wagombea urais utaanza Februari mwakani Iowa, miezi 10 kabla ya uchaguzi mkuu kufanywa
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com