Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya Ikungi Jerry Muro akipokea maelezo ya jinsi zoezi la sensa linavyoendelea katika halmashauri ya ikungi mapema hii leo RC Serukamba na DED wa Ikungi Justice kijanzi akishuhudia uhalisia na ugumu wa zoezi la sensa wakitembea kwa miguu mtaa kwa mtaa katika halmashauri ya Ikungi RC Serukamba akizungumza na Wasimamizi wa Makarani Wa Sensa halmashauri ya Ikungi kabla ya kuaanza kutembelea kaya kwa kaya kukagua zoezi hilo.
![]() |
Karani wa sensa Skovia Deus kutoka ofisi ya Takwimu ikungi akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa Peter Serukamba ya kaya alizozifikia hadi sasa |
![]() |
Karani katika ubora wake akiwajibika |
![]() |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi Justice Kijazi akitoa taarifa ya kaya zilizokwisha hesabiwa hadi kufikia jana agosti 26 ambapo ni kaya 51,109 Sawa na asilimia 85.3% 59,911 |
![]() |
Mzee Rashid mkazi wa Ikungi akisalimiana na RC Serukamba baada ya kushiriki zoezi la sensa |
Na Hamis Hussein - Singida
Mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba amewataka wasimamizi
wa makarani wa sensa waliomaliza kufanya madodoso katika maeneo waliopangiwa
kuwahamisha kwenda kuongeza nguvu maeneo mengine ambayo bado zoezi la sense halijawafikia.
RC Serukamba amesema hayo baada ya kukagua zoezi la sensa
kwenye kaya za Singida Mjini, Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na Itigi Mkoani
humo ambapo amesisitiza kamati za sensa za kila halmashauri kuongeza kasi ya
kuzifikia kaya hadi kufikia jumatatu ya agosti 29 ili kufanikisha zoezi hili.
“Zoezi linaenda
vizuri sana, na utaona tumeshaandikisha watu wengi sana Halmashauri zingine
zimefikia asilimia 80% ukiacha halmashauri ya itigi ambayo inachangamaoto ya
geografia yao ya umbali hivyo kuwalazimu makarani kutembea umbali mrefu lakini
tumeweza kuwajazia mafuta kwenye pikipiki ili wazifikie kaya nyingi”.
Alisema RC Serukamba.
Ameongeza kuwa ili kuongeza kasi hiyo ya kuandikisha kaya
nyingi Zaidi wasimamizi wa sensa pamoja na waratibu wawe karibu kuwafuatilia
makarani ili watakapomaliza maeneo waliopangiwa wahamishiwe kwenye kaya zingime
ambazo hazijafikiwa.
“Msisitizo wangu
nimewambia ni kuwa wale makarani waliomaliza zile kaya walizopangiwa wahamishiwe kwenye kaya zingine nimewaambia
maafisa takwimu wa wilaya kufanya hilo na tumeona kote nilikopita wapo makarani
ambao wamemaliza kaya walizopangiwa na wamepewa kaya zingine nia yetu ni kutaka
tusaidiane ili tuweze kumaliza vizuri”. Aliongeza RC Serukamba.
Mratibu wa Sensa mkoa wa Singida Naing’oya Kipuyo amesema
kuwa kuletwa kwa vifaa vya kuchajia vishikwambi pamoja na kutumia bakaa ya
fedha kwaajili ya kuwawekea makarani mafuta ili kuzifikia kaya zilizopo mbali imeongeza kasi ya uandikishaji wa kaya
ukilinganishwa na hapo awali ambapo karani alikuwa analazimika kuacha zoezi
hilo kutokana na umbali na vishikwambi kukosa chaji.
“Serikali imetoa
ruhusu ya kutumia bakaa ya fedha kurahisisha zoezi hili waratibu wa sensa wa
Wilaya ama kwenye Halmashauri wamekuwa wakikodisha jenereta na pikipiki na
kuweka mafuta kuhakikisha zoezi
linamalizika katika siku saba ambazo zimepagwa tofauti na hapo awali ambapo
makarani hasa wa maeneo ya pembezoni
ilikuwa ikifika saa sita mchana chaji imeisha na kusimamisha zoezi
anaenda kulala mpaka Kesho” alisema Kipuyo.
Katika Halmashauri ya Ikungi Mkurugenzi Justice Kijazi
amesema kuwa kufikia jana agosti 26 tayari kaya 51,109 Sawa na asilimia 85.3%
59,911 lakini akitaja changamoto ambazo zimejitokeza kwenye zoezi hilo ikiwa ni
pamoja na kuzima na kuharibika kwa vishikwambi, baadhi ya wananchi kugoma
kuhesabiwa, pamoja na mwingiliano wa mipaka kati ya Wilaya na wilaya, Kata na
kata na kusema kuwa changamoto hizo zimeshapatiwa ufumbuzi.
Kwa upande wake mratibu wa Sensa wa Halmashauri ya Itigi
Sophia Selemani amesema katika kuzitatua changamoto zinapelekea zoezi hilo
kususa tayari wamepokea Vitunza Chaji
Power Bank 80 huku akiomba kuongezewa kwa Vitunza Chaji 40 ili kukidhi mahitaji
na kuongeza licha changamoto ya Jeografia wanaokumbana nayo lakini kufikia jana
Agosti 26 tayari wameshazifikia kaya 20,694 sawa 71.4% kati ya kaya 28,992.
0 comments:
Post a Comment