METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, January 8, 2020

Taasisi na Mshirika ya Umma 13 Yatekeleza Agizo la JPM

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (Mb)akisisitiza umuhimu wa Taaisisi za Serikali ambazo hazijawsilisha gawio na michango yake katika mfuko mkuu wa Serikali kufanya hivyo kabla Januari 23, 2020 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa mwishoni mwa mwaka 2019 wakati akipokea gawio na michango kutoka kwa Taasisi na Mshirika ya umma na yale yanayomilikiwa kwa ubia na Serikali.


.............


Na Mwandishi
Taasisi na Mashirika ya Umma 13 yatekeleza Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa gawio na michango Serikalini.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma wakati akipokea gawio na michango ya Taasisi hizo, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema kuwa Taasisi 36 ambazo bado hazijatekeleza agizo hilo zifanye hivyo kabla ya Januari 23, 2020.


“ Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi wa Mashirika na Taasisi zote ambazo kufikia tarehe 23 Januari, 2020 zitakuwa hazijawasiliha gawio au michango yao wajiondoe wenyewe katika nafasi zao kwa kushindwa kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli “; alisistiza Dkt . Mpango
Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbutuka akieleza hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa mwishoni mwa mwaka 2019 wakati akipokea gawio na michango kutoka kwa Taasisi na Mshirika ya umma na yale yanayomilikiwa kwa ubia na Serikali.


Katika kipindi cha Desemba 12, 2019 hadi Januari 7, 2020 jumla ya shilingi Bilioni 8.7 zimepokelewa kama gawio na michango ya Taasisi za Serikali na zile ambazo Serikali inazimiliki kwa ubia na wawekezaji.


Wakati katika kipindi cha Novemba 15, 2019 hadi Desemba 11, 2019 jumla ya shilingi Bilioni 12.1 zimekusanywa katika kutoka katika Taasisi na Mashika kama michango yao na gawio.


Akifafanua Dkt. Mpango amesema kuwa fedha zinazokusanywa kutokana na gawio na michango kutoka katika mashirika na taasisi hizo zinatumika katika kuwaletea wananchi maendeleo ikiwemo uboreshaji wa huduma mbalimbali zinazolenga kuchochea ustawi wa wananchi.


Aidha, Dkt. Mpango aliziagiza Taaisisi zote za Serikali kuongeza tija katika utendaji wake ili ziongeze gawio wanalotoa kwa Serikali na michango yao.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa wanampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa usimamizi mzuri wa rasilimali za Taifa kwa maslahi ya wananchi wote.


“ Sasa ni wakati wa wananchi kupata huduma mbalimbali kutokana na fedha zilizowekezwa katika mashirika na Taasisi za Serikali na zile tulizowekeza kwa ubia”; Alisisitiza Dkt. Kijaji
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akisisitiza umuhimu wa Taasisi za Serikali kuchangia maendeleo ya Taifa kwa kutoa gawio na michango ili kuboresha huduma kwa wananchi.


Kwa upande wake msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbutuka amesema kuwa jumla ya Shilingi Bilioni 20.8 zimekusanywa kama gawio na michango kutoka kwa Taasisi na Mashirika ya Umma kati ya Novemba 25, 2019 na Januari 7, 2020.


Aliongeza kuwa Taasisi 36 hazijatoa gawio wala michango yake kati ya 187 zilizotakiwa kufanya hivyo baada ya agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.


Mashirika na Taasisi za Serikali kuwasilisha gawio na michango ni jukumu linalopaswa kutekelezwa na wenyeviti wa bodi na wakurugenzi wa mashirika hayo ili kuchochea maendeleo na ustawi wa wananchi.
Wenyeviti wa Bodi, Wakuu wa Taasisi na watendaji wengine wa Taasisi za Serikali na zile ambazo zinamilikiwa kwa ubia na Serikali wakiwasilisha hundi za mfano leo Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuwasilisha gawio na michango kwa Serikali ikiwa ni utekelezaji wa agizo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa mwishoni mwa mwaka 2019 wakati akipokea gawio na michango kutoka kwa Taasisi na Mshirika ya umma na yale yanayomilikiwa kwa ubia na Serikali.

(Picha zote na Frank Mvungi)
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com