METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, July 16, 2015

Ufaulu kidato cha sita shule za serikali juu.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde, akitangaza matokeo ya kidato cha sita.Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde, akitangaza matokeo ya kidato cha sita.



WATAHINIWA 38,853 kati ya watahiniwa 40,753 waliofanya mtihani wa Kidato cha Sita kwa mwaka 2015, wamefaulu mitihani yao ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.67 ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.
Akitangaza matokeo hayo mjini hapa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde alisema watahiniwa waliofaulu ni asilimia 97.65 ukilinganisha na watahiniwa 38,905 ambao ni asilimia 95.98 wa mwaka jana.
Katika matokeo ya mwaka huu, watahiniwa waliofaulu, wasichana ni 11,737, sawa na asilimia 98.56 wakati wavulana ni 27,119 ambayo ni asilimia 97.27.
Akizungumzia matokeo ya watahiniwa wa shule, Msonde alisema watahiniwa 34,777 ambao ni sawa na asilimia 98.87 walifaulu mitihani yao ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.61.
Wasichana wakiwa ni 10,576 sawa na asilimia 99.46 na wavulana ni 24,201 sawa na asilimia 98.61. Kwa mwaka jana watahiniwa 34,645 ambao ni asilimia 98.26 walifaulu mitihani yao.
Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, Msonde alisema watahiniwa 4,076 sawa na asilimia 88.34 wamefaulu mitihani yao. Mwaka jana watahiniwa 4,260 ambao ni asilimia 80.73 walifaulu mitihani yao.
“Kuimarika kwa ufaulu wa watahiniwa wa Kidato cha Sita mwaka huu ikilinganishwa na mwaka 2014 ni sehemu za juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha mazingira ya elimu nchini.”
Akizungumzia madaraja ya ufaulu, Msonde alisema watahiniwa 31,450 ambao ni asilimia 89.41 wamefaulu katika daraja la juu ya Distiction, Merits na Credit, wasichana wakiwa ni 9,876 na wavulana 21,574.
Aidha, Msonde alisema takwimu za matokeo zinaonesha kuwa ufaulu wa watahiniwa wa shule katika masomo ya Historia, Jiografia, Kiingereza, Fizikia, Kemia na Bayolojia umepanda ukilinganisha na mwaka jana huku ufaulu wa juu ni wa masomo ya Historia na Kiswahili ambao ni asilimia 99.96.
Alisema ufaulu wa masomo ya sayansi ya Kemia na Fizikia umeimarika ukilinganisha na mwaka jana huku ufaulu wa masomo ya Maarifa, Kilimo, Hisabati ukishuka kidogo.
Kwa upande wa shule 10 bora zilizofanya vizuri, Msonde alizitaja kuwa ni Feza Boys, Runzewe, Feza Girls, Sumbawanga, Ivumwe, St Marys’ Mazinde Juu, Vwawa, Kisimiri, Namabengo na Scolastica.
Alisema shule 10 zilizofanya vibaya kuwa ni Bariadi, Ilongero, Lwangwa, Kilangalanga, Kaliua, Lugoba, Iwalanje, Mtwara (Ufundi), Kwiro na Meta. “Tathmini inaonesha kwamba shule kumi bora kitaifa, shule tano ni za serikali na tano zisizo za Serikali, katika shule 20 bora kitaifa, shule 13 za Serikali na saba ni zile zisizo za Serikali,” alisema.
Aidha aliwataja wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi kuwa ni Ramadhani Ngembe (Feza Boys), Lesian Lengare (Ilboru), Hunayza Mohamed (Feza Boys), Rosemary Chengula (St Mary’s Mazinde Juu), Kevin Rutahoile na (St Joseph Cathedral), Anderton Masanja (St. Joseph Cathedral), Joseph Pasian (Ilboru), Lupyana Kinyamagoha (Mzumbe), Yonazi Senkondo (Feza Boys), Meghna Solanki
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com