METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, January 30, 2024

DKT.DUGANGE:VIKUNDI 345 VIMEKIDHI VIGEZO VYA KUPEWA ZABUNI


NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Mhe Dkt Festo Dugange amesema Serikali za Mitaa zimeweka utaratibu wa kusajili makundi maalum ya wanawake, vijana na wenye ulemavu ambapo ameeleza zaidi ya vikundi maalum 345 vimesajiliwa katika halmashauri ambavyo vimekidhi vigezo vya kupewa zabuni.

Mhe Dkt Dugange ametoa kauli hiyo leo wakati akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha kwanza cha mkutano wa 14 wa Bunge la 12 ulioanza leo jijini Dodoma.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Shally Raymond aliyeuliza ni Zabuni ngapi zilizotolewa na Halmashauri za Majiji, Manispaa na Wilaya kwa makundi maalum hasa Wanawake kama sheria inavyotaka, Mhe Naibu Waziri Dkt Dugange amesema,

“ Kwa mujibu wa sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka  2011 ma marekebisho yake ya mwaka 2016 katika kifungu cha 64 (2) (c) na tangazo la Serikali Na. 333 la mwaka 2016, taasisi zinapaswa kutenga asilimia 30 ya manunuzi kwa ajili ya makundi maalum.

“ Mamlaka ya serikali za mitaa imeweka utaratibu wa kusajili makindi maalum. Aidha vikundi zaidi ya 345 vimesajiliwa katika Halmashauri. Jumla ya vikundi 228 vya malundi maalum vilipewa zabuni mbalimbali katika mamlaka ya serikali za mitaa. Katika zabuni hizo vikundi 70 vilikua vya wanawake,” Amesema Mhe Dugane.

Aidha Mhe Dugange amesema serikali itaendelea kutenga bajeti na kutoa vibali vya ajira kwa maafisa watendaji wa vijiji, mitaa na kata kulingana na mahitaji kote nchini.

Mhe Dugange amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Hawa Mwaifunga aliyehoji utaratibu unaotumika kuajiri watendaji kwenye halmashauri nchini.

“ Utaratibu unaotumika kuajiri maafisa watendaji wa vijiji/mitaa na kata ni kama ifuatavyo. Mamlaka za serikali za mitaa zinatenga fedha za mishahara kwenye bajeti na kuomba kibali cha ajira kwa Ofisi ya Rais-Utumishi na baada ya kupata kibali mamlaka za serikali za mitaa zimekasimiwa jukumu la kutangaza na kuwafanyia usaili waombaji, kuwaajiri na kuwapangia vituo vya kazi waliokidhi vigezo vya ajira,” Amesema Mhe Dkt Dugange.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com