Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameitaja Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), kuongeza jitihada katika kushirikiana na wadau wote wa masuala ya vijana nchini katika afua za kudhibiti UKIMWI kwa Vijana.
Waziri Ndalichako ameyasema hayo leo tarehe 30 Novemba, 2023 wakati wa kilele cha shuguli za Vijana kuelekea Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani Mkoani Morogoro..
Aidha amewasihi vijana wote nchini, kujikinga na ugoonjwa ili kujikinga na maambukizo ya VVU.
“Wale mlio shuleni na vyuoni hakikisheni mnaweka mkazo katika Elimu na kujiepusha na tabia zote hatarishi zinazopelekea kupata maambukizo ya VVU.”
Vilevile Profesa Ndalichako ametoa rai kwa wadau wote wa masuala yanayo husu vijana walio shuleni/vyuoni na nje ya shule kuweka mkazo katika utoaji wa elimu inayohusu VVU na UKIMWI.
0 comments:
Post a Comment