Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mwantum Mgonja Leo June 26, 2023 amekabidhiwa rasmi ofisi huku akiomba ushirikiano kwa Watumishi, Wakazi na Wananchi wa Manispaa hiyo
Mkurugenzi huyo amekabidhiwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu. Athuman Msabila kabla ya kuhamishiwa Halmashauri ya Wilaya Igunga Mkoani Tabora.
Mkurugenzi huyo amekabidhiwa Mbele ya Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Wakuu wa idara na Vitengo, na Watumishi wengine kutoka idara na vitengo mbalimbali vya Halmashauri
Meya Wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Baraka Naibuha Lupoli amempongeza Mkurugenzi aliyehamishwa kwa namna alivyokuza Mapato ya Ndani kwa kipindi cha Miaka miwili huku akitekeleza miradi ya Maendeleo kwa mapato ya Ndani kama ujenzi wa Ofisi za kata, Zahanati, na Uendelezaji wa Zao la Mchikichi
Pia amempongeza Mkurugenzi mpya kwa kupangiwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji huku akiahidi kutoa ushirikiano kwa kuhakikisha ukuaji wa mapato ya ndani na uanzishaji wa miradi kwa mapato ya ndani
0 comments:
Post a Comment