METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, June 28, 2023

MBUNGE HASHAM AISHAURI SERIKALI KUONGEZA NGUVU YA WAUGUZI NA VIFAA TIBA KATIKA VITUO VYA AFYA


Na Saida Issa,Dodoma

BAADA ya kupita kwa bajeti kuu ya serikali ya mwaka wa fedha 2023/24  iliyopitishwa na Bunge kwa asilimia 95 Mbunge wa jimbo la ulanga mhe. Salim Alaudin Hasham ameishauri serikali kuongeza nguvu katika utoaji wa huduma kwenye vituo vya afya nchini.

Akizungumza katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma amesema vituo vya afya vimejengwa kwa wingi nchini lakini ni vyema kasi hiyo ikaendana na kuongeza watoa huduma za afya na vifaa tiba na dawa ili viendane na majengo yaliyopo.

“kupita kwa bajeti kuu ya serikali ni jambo moja lakini kutekeleza ni jambo jingine kwani tunakwenda kufaidika kwenye sekta ya afya, majengo tunafahamu yapo mengi lakini kunahitajika nguvu kwakuongeza wahudumu wa afya pamoja na vifaa tiba” amesema mbunge huyo.

Akizungumza kuhusu uwekezaji wa Bandari amesema kuwa ni haki ya wananchi kuzungumzia uwekezaji huo kwani ni haki yao lakini kinachoonekana ni wananchi kuendelea kupewa elimu juu ya uwekezaji na hii itasaidia kufahamu ukweli badala yakusikiliza taarifa zinazotolewa kwenye mitandao ya kijamii ambazo nyingine ni upotoshaji.

“wanaopiga kelele ni wananchi ambao kimsingi ni haki yao kufanya hivyo kwasababu bandari ni mali yao lakini nafikiri hawana uelewa wa kutosha lakini pia kwaupande wa serikali inatakiwa kutoa elimu zaidi kuwaelewesha juu ya swala la bandari”amesema mbunge huyo.

Aidha amesema nchi kubwa zinazoendelea bado zinategemea wawekezaji katika kuwekeza ili wapate maendeleo ya nchi.

Katika hatua nyingine amewashukuru wananchi wa ulanga kwakumuamini na kumchagua huku akisema kuwa tangu aingie madarakani amefanikiwa kufanikisha ahadi zilizotolewa na serikali kwa asilimia 50 hadi 60 na zile ahadi za vyanzo binafsi amefanikiwa kutekeleza kwa zaidi ya asilimia 90.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com