Mkuu wa Wilaya ya pangani Mhe. Zainab Abdallah akieleza jambo kuhusu wilaya yake wakati wa kikao hicho.
Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akisalimiana na
Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu Bw. Kayanda Ibrahim
alipowasili wilaya ya Pangani kwa ajili ya ziara kukgua utekelezaji wa
masuala ya UKIMWI na wenye ulemavu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akizungumza masuala ya watu wenye
ulemavu wakati wa kipindi maalum cha elimu kwa umma katika studio za
radio Pangani iliyopo Wilaya ya Pangani mkoani Tanga alipofanya ziara
yake katika Taasisi ya UZIKWASA Mkoani humo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akizungumza jambo wakati wa kikao
chake na watendaji wa Taasisi ya UZIKWASA (hawapo pichani) alipokutana
nao Oktoba 3, 2019 ili kukagua kazi wanazotekeleza.
Katibu Tawala wa
Pangani, Mwalimu Hassan Nyange akifafanua jambo wakati wa kikao cha
uwasilishwaji wa taarifa za Wilaya hiyo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani).
Mkurugenzi wa Taasisi ya UZIKWASA Bw. Novatus Urassa akieleza jambo wakati wa kikao hicho.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
**************************************
NA.MWANDISHI WETU
Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masualaya ya Watu Wenye Ulemavu
Mhe. Stella Ikupa amewaasa watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa za
mikopo zitolewazo na Serikali pamoja na wadau mbalimbali ili ziwasaidie
kuboresha maisha yao.
Ametoa wito huo
hii leo (oktoba 3, 2019) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
katika kipindi maalum kinachorushwa na radio Pangani alipotembelea
kituoni hapo Mkoani Tanga ili kujionea jitihada zinazofanya na radio
hiyo katika kuhabarisha umma juu ya masuala mtambuka ikiwemo vipindi
maalum vya elimu ya jamii kuhusu masuala ya watu wenye ulemavu nchini.
Mhe.Ikupa
alieleza kuwa Serikali imeendelea kuhakikisha inatekeleza sheria namba 9
ya mwaka 2010 inayohusu haki na ulinzi kwa watu wenye ulemavu na
kuhakikisha wanapatiwa haki hizo ikiwemo masuala ya ajira, elimu, afya
na utengamao wa maisha yao ili kuondokana na dhana potofu ya utegemezi
kwa kundi hilo.
“Kwa muda mrefu
sasa watu wenye ulemavu nchini wamekuwa wakinyanyaswa na kunyimwa haki
zao za ajira, elimu, afya na kufikia wakati jamii kuwaficha badala ya
kuwapa nafasi ya kuonesha uwezo wao na kuweza kushiriki katika shughuli
za uzalishaji mali ili waweze kujikwamua kiuchumi kuondokana na hali ya
utegemezi.”alisema Mhe. Ikupa.
Aliongezea kuwa
tayari Serikali imeendelea na jitihada za kuwawezesha watu wenye ulemavu
kwa kuwatengea asilimia 2 katika kila Halmashauri nchini ambazo
zinatumika katika kuwapatia mikopo kwa kupitia uundwaji wa vikundi na
kujisajili ili kupewa mikopi hiyo isiyokuwa na riba na kujikwamua
kiuchumi.
Naye Mkuu wa
Wilaya hiyo Mhe. Zainab Abdallah alieleza kuwa Wilaya yake inatekeleza
hilo na kuwataka vijana wenye ulemavu kutumia fursa za mikopo ili
kuwezeshwa na kujiendeleza weneywe.
Akiongezea kuwa,
jitihada za Wilaya yake ni kuhakikisha wanawafikia wenye ulemaviu
katika kuwapatia mahitaji yao ikiwemo, elimu na kuwapa nafasi katika
fursa mbalimbali zinazojitokeaza katika Wilaya yake.
“Niwaombe
muendelee kujiunga kwenye vikundi kwani kasi iliyopo hairidhishi kwa
kuwa hadi sasa kuna vikundi vitatu tu ambavyo vimesajiliwa Halmashauri
na ili uweze kupata mikopo hiyo ni lazima vikundi vitambulike,”alieleza
Zainab.
Aliongezea kuwa,
ipo haja ya kila mwenye ulemavu kujitahidi kujishughulisha katika
shughuli ya kumuongezea kipato kwa kuzingatia uwezo aina ya ulemavu wake
kwa kuwa serikali imeendelea kuweka mkazo katika kuliangalia kundi
hili.
“Hadi sasa Wilaya
yetu ina watu wenye ulemavu zaidi ya 700 hivyo ni wakati sahihi kuona
namna kundi hili linaangaliwa na kupatiwa elimu ya ujasiriamali ili
waweze kujikimu katika mahitaji yao na familia zao kwa
ujumla’”alifafanua Mhe. Zainab
Kwa upande wake
Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Hassani Nyange alimpongeza Naibu waziri
huyo kwa jitihada anazozifanya katika kuhakikisha kundi la wenye ulemavu
linapatiwa huduma kwa usawa na haki ili kuendelea kuboresha mazingira
ya kundi hilo.
“Binafsi
ninafuraha kwa ujio wako Pangani tunaahidi kuendelea kuunga jitihada za
serikali vya vitendo kwa kuzingatia awamu hii ya tano imejikita kuinua
uchumi kuanzia mtu mmoja mmoja hadi Taifa kwa ujumla hivyo tutaendela
kuhakikisha kila mwananchi anashiriki katika shughuli za uzalishaji mali
na kufikia Taifa la uchumi wa kati,”aliongezea Nyange.
0 comments:
Post a Comment