METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, May 19, 2023

TCRA KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA WAHALUFU WA MITANDAONI



  Na Saida Issa, Dodoma

MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania TCRA kwakushirikiana na Jeshi la polisi katika kudhibiti utapeli wamekuwa wakidhibiti watoa huduma kwakufuata miongozo katika kusajili na kuhakiki laini za simu huku wanaoibia watu kupitia mitandao wamekuwa wakichukuliaa hatua za kisheria.

Hayo yameelezwa katika viwanja vya Bunge jijini dodoma katika maonyesho ya Banda la taasisi hiyo yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Lucy Mbogoro Mkuu wakitengo cha mawasiliano na mahusiano kwa umma Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) amesema kuwa tangu kukamiliza kwa zoezi la uhakiki na usajili laini za simu tarehe 13.4.2023 amesema zoezi hili limefanikiwa kudhibiti wizi nawale wote wanaofanya uhakifu mtandaoni watakamatwa.

Aidha Kuhusu usafirishaji wa vifurushi na vipeto Lucy amesema kuwa ili kuepuka kutapeliwa nakuepuka kupoteza bidhaa zao nivyema wananchi wakatumia watoa huduma waliosajiliwa namamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA

"Tunapenda kuwaarifu wananchi kuwa ili kuepuka kutapeliwa na kuepuka kupoteza bidhaa zao ni vyema kutumia watoa huduma waliosajikiwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania,"amesema.

Pia Kuhusu kutuma vitu ambavyo ni hatarishi na hatamu amesema TCRA imekua ikifanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha mzigo unaosafirishwa hauna athari kwa wengine kama anavyoeleza.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 ili kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com