METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, May 19, 2023

SERIKALIA YAIPONGEZA TTCL KWA KUENDELEA KUBUNI HUDUMA ZINAZOCHOCHEA MAENDELEO NCHINI



  
   Na Saida Issa, Dodoma

SERIKALI imelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ,kwa kuendelea kubuni huduma zinazochochea maendeleo ya sekta ya Mawasiliano hapa nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson wakati alipotembelea na Kukagua Banda la Shirika hilo lililopo katika Maonesho yaliyoandalaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ,kwa taasisi zilizopo Chini yake yanayoendelea katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Spika Dkt.Tulia amesema Shirika hilo limejipambanua katika utoaji wa huduma zake za Mawasiliano ambapo kwa sasa wameweza kufikisha huduma za Mawasiliano katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Aidha Dkt.Tulia amesema kuwa TTCL imeifungua nchi kidijitali jambo ambalo limesaidia kuchochea maendeleo ya Mtu mmoja mmoja na taifa Kwa ujumla.

"TTCL wameifungua nchi Kimawasiliano ukweli huo lazima tuusema Kwanza hili la kupeleka huduma ya Mawasiliano katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro ni jambo la kupongezwa Kwa nguvu zote Kwani sasa Kila mmoja anaweza kuwasiliana na ndugu na jamaa wakiwa hata huko huko kileleni haya ni maendeleo, "amesema Dkt.Tulia

Kadhalika amezungumzia  huduma zinazotolewa na Shirika hilo za Majumbani ikiwemo huduma ya Fiber Nyumbani Kwako na Smart home kuwa zinasaidia kurahisisha Mawasiliano na kusimamia ulinzi na Usalama.

Huku Meneja wa Biashara wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Jijini Dodoma Leyla Pongwe, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika hilo,amesema kuwa Kasi ya Shirika hilo katika kuleta mapinduzi ya Kimawasiliano ni kutaka kuhakikisha agenda ya Serikali inafanikiwa ya kutaka kufikia Uchumi wa Kidijitali ifikapo 2025.

"Serikali ina malengo ya kuhakikisha uchumi wa kidijitali unakuwa kwa kasi ifikapo 2025 sasa Jukumu letu kama Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL ni kufungua njia kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa,"amesema

Amesema TTCL imekuja na huduma Mpya yenye malengo ya kurahisisha upatikanaji wa huduma ya Mawasiliano na Usalama Kwa mtumiaji wa huduma hiyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com