METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, May 20, 2023

Mhe. Eng. Kundo Mathew awataka wakandarasi kukabizi jengo la Umoja ya Posta Afrika kabla ya Juni 20



 







Na Innocent Natai-Arusha

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Eng. Kundo Methew amewataka Wakandarasi wanaojenga jengo la Umoja wa Posta Afrika (PAP) linalojengwa Mkoani Arusha kuhakikisha ujenzi wa jengo unakamilika kabla ya Juni 20/2023 ili kuziachia taasisi zinazotumia jengo hilo kuanza maandalizi ya Uzinduzi

Eng. Kundo ameyasema hayo leo Mei 20,2023 alipofanya ziara ya kuangalia ujenzi wa jengo hilo Mkoani Arusha, ambapo amesema kuwa wanatarajia Mwezi Agosti 2023 jengo hilo litazinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, 

Hivyo sekta husika zinazotumia jengo hilo ambao ni Umoja wa Posta Afrika(PAP) na Wizara ya Habari na Teknolojia ya Habari ambao ni washiriki wakubwa kupitia Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) wanatakiwa kukabidhiwa jengo hilo likiwa limekamilika ili kuanza taratibu mbalimbali ikiwemo Mialiko ya wanaohudhuria katika uzinduzi

Akizungumzia maendeleo ya ujenzi huo amesema kuwa mpaka sasa ujenzi umefikia hatua nzuri ambapo miundombinu ya ujenzi imefikia Asilimia 98.5% hivyo matarajio ni kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya Wiki Mbili 

“Tumepita kila mahali pale penye changamoto tumewaelekeza wafanye nini lengo letu ni kwamba Mweshimiwa Rais anapokuja kuzindua jengo hili liwe katika picha ya kimataifa, picha ambayo sisi kama Tanzania tunakwenda kujitangaza kwenye masuala ya Mawasiliano” alisema Mhe. Eng. Kundo

Amebainisha kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kikamilifu kutakwenda kuvutia taasisi nyingine za kimataifa kuvutiwa kujenga majengo yao kwani kupitia uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan umefungua milango ya kimataifa kuja kuwekeza nchini 

Jengo hilo lenye ghorofa Kumi na sita (16) linajengwa kwa Ushirikiano wa Umoja wa Posta Afrika(PAP)  na Serikali ya Tanzania ambapo serikali ya Tanzania inachangia asilimia 40% na Umoja wa Posta Afrika(PAP) wanachangia asilimia 60% ya Ujenzi na linatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2023

Katika ziara hiyo aliambatana na  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Ndg.Selestine Gervas Kakele

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com