Na Innocent Natai-Arusha
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Eng. Kundo Methew amewataka Wakandarasi wanaojenga jengo la Umoja wa Posta Afrika (PAP) linalojengwa Mkoani Arusha kuhakikisha ujenzi wa jengo unakamilika kabla ya Juni 20/2023 ili kuziachia taasisi zinazotumia jengo hilo kuanza maandalizi ya Uzinduzi
Hivyo sekta husika zinazotumia jengo hilo ambao ni Umoja wa Posta Afrika(PAP) na Wizara ya Habari na Teknolojia ya Habari ambao ni washiriki wakubwa kupitia Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) wanatakiwa kukabidhiwa jengo hilo likiwa limekamilika ili kuanza taratibu mbalimbali ikiwemo Mialiko ya wanaohudhuria katika uzinduzi
Akizungumzia maendeleo ya ujenzi huo amesema kuwa mpaka sasa ujenzi umefikia hatua nzuri ambapo miundombinu ya ujenzi imefikia Asilimia 98.5% hivyo matarajio ni kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya Wiki Mbili
“Tumepita kila mahali pale penye changamoto tumewaelekeza wafanye nini lengo letu ni kwamba Mweshimiwa Rais anapokuja kuzindua jengo hili liwe katika picha ya kimataifa, picha ambayo sisi kama Tanzania tunakwenda kujitangaza kwenye masuala ya Mawasiliano” alisema Mhe. Eng. Kundo
Amebainisha kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kikamilifu kutakwenda kuvutia taasisi nyingine za kimataifa kuvutiwa kujenga majengo yao kwani kupitia uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan umefungua milango ya kimataifa kuja kuwekeza nchini
Jengo hilo lenye ghorofa Kumi na sita (16) linajengwa kwa Ushirikiano wa Umoja wa Posta Afrika(PAP) na Serikali ya Tanzania ambapo serikali ya Tanzania inachangia asilimia 40% na Umoja wa Posta Afrika(PAP) wanachangia asilimia 60% ya Ujenzi na linatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2023
Katika ziara hiyo aliambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Ndg.Selestine Gervas Kakele
No comments:
Post a Comment